Saturday, May 30, 2009

Vijidudu vya Malaria Vyashinda Dawa!


Wataalamu wa tiba wa kimataifa wamesema kuwa wamepata uthibitisho wa kwanza kuhusiana na kushindwa nguvu dawa muhimu ya kwanza duniani ya kutibu malaria na vijidudu vinavyosababisha ugonjwa huo. Wamesema uchunguzi uliofanywa magharibi mwa Cambodia kuhusiana na suala hilo unapaswa kuzingatiwa, kwani kushindwa kikamilifu dawa hiyo kutasababisha maafa makubwa ya kiafya duniani. Imeonekana kuwa dawa za kutibu malaria zinachukua muda mrefu kuua vijidudu vya malaria katika damu ya mgonjwa kuliko huko nyuma.
Uchunguzi huo ni tahadhari ya mapema ya kushindwa dawa ya kutibu malaria katika maeneo mengi zaidi, ugonjwa ambao unaua mamilioni ya watu kila mwaka duniani.