Sunday, June 6, 2010

Kensa kuua watu milioni 13.2 ifikapo mwaka 2030


Maafisa wa Umoja wa Mataifa wametangaza kwamba, watu zaidi ya milioni 13.2 watafariki dunia ifikapo mwaka 2030 kutokana na maradhi ya kensa, idadi ambayo ni mara mbili ya ile ya mwaka 2008. Takwimu hizo za hivi karibuni zinaonyesha pia kwamba, ugonjwa wa saratani mwaka 2008 ulisababisha watu milioni 7.6 waage dunia na kwamba kesi mpya milioni 12.7 za kensa mbalimbali zimegunduliwa mwaka huu. Nchi zinazoendelea zimeripotiwa kuwa na asilimia 56 ya kensa mpya na asilimia 63 ya kensa zote zilizoripotiwa mwaka 2008. Kensa ambazo zilitokea kwa kiasi kikubwa mwaka 2008 ni kensa za mapafu, matiti na kensa ya utumbo, rectum na apendeksi au colorectal cancer. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Kimataifa cha Utafiti wa Kensa( IARC) kesi za ugonjwa wa kensa zitaongezeka mara dufu katika miongo miwili ijayo iwapo hali ya sasa itaendelea hivyo hivyo. Christopher Wild Mkurugenzi wa IARC amesema kwamba, maradhi ya kensa hakuna sehemu yoyote duniani yasipokuwepo, hata katika nchi zilizoendelea na zenye utajiri mkubwa. Amesisitiza kwamba la kusikitisha ni kuwa maradhi ya kensa ambayo mwanzoni yalishudiwa kwa wingi katika nchi zinzoendelea hivi sasa yapo pia katika nchi masikini.

1 comment:

Disminder orig baby said...

eee Mungu tunusuru, tutakufa wengi jamani. Shida na lishe zisizo na mpango, hakuna mazoezi ni kazi ngumu tu za kuchosha miili then unaishia kula chakula hata hakina kirutubisho.