Kwa
mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na kutangazwa na Shirika la Afya Duniani
WHO katika mkutano wake wa tarehe 19-22 Juni 1946 na kusainiwa na wawakilishi
wa nchi 61 duniani, 'afya ni hali ya mtu kuwa vizuri kimwili, kiakili na
kijamii na sio tu kutokuwa na ugonjwa au udhaifu.' Ufafanuzi huo ulianza
kutumika Aprili mwaka 1948 na hadi hii leo maana hiyo ya afya haijabadika.
Ufafanuzi huo unamaanisha kwamba, tunaposema mtu ana afya sio tu tunakusudia
kuwa mwili wake hauna maradhi, upungufu au udhaifu bali pia mtu huyo anatakiwa
asiwe na matatizo ya kimwili, kiakili na hata kijamii. Kwa mujibu wa tafisri
hiyo pana ya neno 'afya' tunaona kuwa watu wengi wanaamini kuwa afya imeganyika
katika makundi mawili muhimu ambayo ni afya ya kimwili na afya ya kiakili. Afya
ya mwili kwa binaadamu ina maana, kuwa na mwili wenye afya usiokuwa na maradhi,
afya ambayo kwa kawaida hutokana na kuupa mwili mazoezi ya mara kwa mara, lishe
bora na mapumziko ya kutosha. Katika nchi au maeneo ambayo watu wanapata lishe
bora, huduma nzuri za afya na kuishi katika hali ya kimaisha inayoambatana na
viwango vinavyotakiwa, kwa kawaida vimo na uzito wao huongezeka. Ukweli ni
kuwa, ukiwauliza watu wengi afya ni nini, watasema kwamba inahusiana na
mwili kuwa salama bila ya kuathirika na ugonjwa. Lakini tukienda ndani
zaidi, kitiba afya ya mwili inaamanisha ustawi wa mwili hali ambayo mtu
anaipata kwa kutekeleza vipengee vyote vinavyohusiana na afya katika maisha
yake. Uzima wa mwili unaakisi kufanya kazi vizuri moyo na mfumo wa kupumua,
uwezo wa misuli, viungo pamoja na mwili kuweza kukubali mabadiliko tofauti na
muundo wa mwili kwa ujumla. Masuala mengine ni pamoja na lishe bora, uzito wa
mwili, kutokuwepo uraibu wa madawa ya kulevya, pombe, mahusiano salama ya kimwili,
usafi kwa ujumla na pia kulala na kuamka kwa wakati unaotakiwa.
Afya ya akili au uzima wa kiakili ni
utambuzi wa mtu na uzima wake kisaikolojia. Mtu ambaye ana afya nzuri ya
kiakili hana matatizo ya kiakili au kichaa. Kwa mujibu wa Shirika la
Afya Duniani WHO, 'afya ya akili ni pale mtu anapoweza kufahamu uwezo
wake na kustahamili mfadhaiko (stress) unaotakana na dhiki au matatizo
ya kawaida ya kimaisha. Aweze kufanya kazi yenye kuleta mafanikio na
kuchangia masuala tofauti katika jamii yake.'
Ni rahisi watu kuelezea maana ya ugonjwa
wa akili kuliko afya ya akili. Watu wengi wanakubali kwamba afya ya
akili ni kutokuwepo ugonjwa wa akili lakini maana hiyo haitoshi. Hii ni
kwa sababu kama tutachagua watu 100 ambao hawana kichaa au ugonjwa wa
akili unaoweza kutambuliwa na daktari wa akili, lakini miongoni mwao
tunaweza kuona kwamba afya ya baadhi yao kiakili imeimarika kuliko
wengine.Tunaweza kusema kuwa, afya ya akili inajumuisha masuala kadhaa
kama vile uwezo wa kuishi kwa furaha, uwezo wa kuvumilia shida na
kurejea katika hali ya kawaida baada ya kupatwa na matitizo, uwezo wa
kuwa na uwiano katika maisha, uwezo wa kubadilika kwa urahisi na kuzoea
mazingira mapya, kujihisi salama na kujitambua.
2 comments:
asante sana sana Mungu akubariki
Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* bahati nzuri
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159
Post a Comment