Wednesday, January 19, 2011

Jibu la swali la Mdau


Kuna mdau ambaye aliniuliza muda mrefu uliopita iwapo mwanamke na mwanamume ambao wana Ukimwi wanaweza kupata mtoto kwa njia ya IVF au la. Kwa kuwa ni muda mrefu sikuwepo kuandika blog hii na kujibu maswali, nimeamua kulijibu swali hili hapa ili muulizaji aone jibu lake kwa urahisi na wengine pia waweze kufaidika nalo.
Jibu ni kuwa ni vigumu kusema kuwa njia hiyo inaweza ku-guarantee kuzaliwa mtoto asiyekuwa muathirika wa HIV, hasa kwa kuzingatia kuwa wote baba na mama ni wagonjwa. Ni kweli iwapo mmoja tu ndiye mgonjwa kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanyika IVF kwa njia inayoitwa Sperm wash ambayo hufanywa kabla ya mbegu ya kiume kutumbukizwa kwenye tumbo la mama na huweza kuzaliwa mtoto asiye mgonjwa wa Ukimwi. Lakini sikukatishi tamaa mdau, iwapo huna matatizo ya uzazi, kuna uwezekano wa mwanamke na mwanamume waathirika wa Ukimwi kuzaa mtoto asiyeathirika, iwapo watakuwa wakitumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo kabla na wakati wa ujazito, na hasa mama kuendelea kutumia dawa hizo wakati wote wa ujauzito.Kuzaliwa watoto wasioathirika kutoka kwa wazazi waathirika wa Ukimwi, kumeshuhudiwa mara nyingi nchini Tanzania na kwingineko.

2 comments:

Anonymous said...

kiukweli umejibu kitu cha uongo na hauna uhakika ....mtt hupata virusi wakati wa kuzliwa na kunyonyesha..sparms hazihusiki kbisa ktk suala zima la maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtt,..ingekuwa hivyo hakuna mtt ambae angepona na pia kungekuwa na dawa za ukimwi

Anonymous said...

Yeah hata mimi hapa nimeshangaa....Hii inabidi ubadili kwavile scientific inawezekana kabisa kuzaa mtoto asiye HIV positive. Mtoto anapata ukimwi pale anapopita katika njia ya mama yake wakati wa kuzaliwa. Na kwa vile ngozi yake ni very delicate ndio maana anapata damu ya mama yake ambayo ina Ukimwi. Sio lazima IVF hata naturally way watu wawili wenye ukimwi wanaweza kuzaa mtoto asiye na ukimwi. Lakini mama anayakaiwa aanze kwenda clinic mara tu anapokua amepata mimba. ITH