Sunday, January 16, 2011

Kuwaanzisha watoto chakula kigumu miezi 6 mapema kunawasaidia


Maneno haya si yangu, lakini nakumbuka kwa uzoefu wangu siku zote nilikuwa nikipingana na waalimu darasani na mahospitalini kuhusu muda wa kuanzishwa chakula kigumu watoto wanaonyonya au 'weaning'!. Siku zote walimu wangu chuo kikuu walikuwa wakisema kuwa watoto wachanga wanaonyesha waanzishwe vyakula vingine wanapokuwa na miezi minne, lakini mie nikipinga na kusisitiza kwamba muda huo utumike kwa watoto wenye asili ya kizungu au weupe, lakini kwa uzoefu wangu, watoto wetu wa Kiafrika tunawaanzisha chakula kigumu wanapokuwa na miezi minne, kwani ifikapo muda huo maziwa ya mama zao huwa hayawatoshi tena! Pia hata wadau wa Kona ya Afya pale waliponiomba ushauri niliwashauri hivyo.
Hoja yangu hiyo imethibitishwa hivi karibuni na timu moja ya Uingereza ambayo ilifanya utafiti na kuchapisha utafiti huo katika Makala ya Tiba ya Uingereza. Wanatimu hiyo wamesema, kutegemea tu maziwa ya mama pekee kwa watoto hadi miezi sita sio vizuri na hayatoshi. Wamesema maziwa ya mama yanaweza kuwa na faida iwapo watoto wataanzishwa vyakula vinginevyo mapema hasa baada ya miezi minne. Huko nyuma wataalamu walishauri kuwa mtoto apewe maziwa ya mama pekee hadi miezi sita lakini hivi sasa wamebadilisha msimamo huo na wanashauri mtoto aanze kupewa chakula kingine akiwa na miezi minne huku akiendelea kunyonyeshwa. Miaka 10 iliyopita Shirika la Afya Duniani lilitoa muongozo kwamba, watoto wachanga wanyonyeshwe maziwa ya mama pekee hadi miezi 6!
Utafiti mwingine umeonyesha kuwa, watoto wachanga wanaocheleweshwa kuanzishwa chakula kigumu hupatwa na upungufu wa damu au anemia kuliko wale wanaoanzishwa vyakula vingine wakiwa na miezi minne hadi 6. Hata hivyo wazazi na walezi wametakiwa kuzingatia aina ya vyakula wanavyowapa watoto wao wachanga pale wanapofikia muda wa kuanza kula, kwani baadhi ya vyakula huwasababishia allergies na pia kufanya wakose choo.

2 comments:

Anonymous said...

mpaka sasa tafiti nyingi zaidi zimeonyesha kuwa kuna faida zaidi kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama tu mpaka miezi 6, na ndio ushauri unaokubalika kwa sasa na shirika la afa duniani. na utafiti unaonesha manufaa kwa watoto wa aina zote, wazungu, waafrika, wahindi, wachina nk.
hizi tafiti zinaonesha manufaa katika "population level" (sijui kiswahili chake) lakini kwa mtoto mmoja mmoja inabidi kuangalia uwezekano kwa sababu watu wako tofauti - akina mama wengine wana maziwa a kutosha wengine sio.

Anonymous said...

Na pia ujue kuwa ukimuanzisha mtoto mapema chakula kuna uwezekano mwingi wa kupata matatizo ya tumbe kuliko yule anayesubiri mpaka utumbo wake ukomae kidogo. Maziwa ya mama yanamtosheleza mtoto mpaka miezi sita kabisa. kam yanatoka vizuri kwa vile kwetu hatuna breast pumps ndio maana watoto wetu wanaanza kulishwa uji mapema sana. Sio kwa vile ni wazungu ni kwa vile wao wana fridges za kuhifadhi maziwa ya mama vizuri na kujua hayataharibika na pia wana breast pumps au wanatumia formula. Hivyo mtoto anauhakika wa kushiba...

halafu kwetu ingawaje ndio wanyonyeshaji wakubwa hatufundishani jinsi ya kunyonyesha na kumake sure mtoto anapata maziwa ya kutosah..As a new mother nilikwenda kwenye lactation class mara mbili na nilipijifungua nilikua na lactation consultant ambaye alikua ni nurse kwa week moja. Ilinisaidia sana na iliengeza supply yangu kwa siku kwa ajili ya technicals zao.