Sunday, May 23, 2010

WHO YATAHADHARISHA JUU YA UNENE WA WATOTO


Mawaziri wa Afya Duniani huku wakitahadharisha juu ya ongezeko la idadi ya watoto wenye unene wa kupindukia, wamesema kwamba watajaribu kupunguza kutumiwa vyakula holela (junk food) kwa kupiga marufuku matangazo ya vyakula hivyo. Mawaziri hao wa nchi 193 duniani ambazo ni wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wametoa muongozi kwa ajili ya mashirika ya kuuza vyakula na vinywaji visivyokuwa na ulevi kwa ajili ya watoto.
Viwanda vya vyakula na vinjwaji vimetakiwa kuongeza udhibiti katika aina zote za mauzo ya vyakula kwa watoto, na wauzaji vyakula wadogo wadogo pia wametakiwa kuacha kuzalisha na kuuza vyakula ambavyo si vizuri kwa afya ya watoto. WHO imesema kwamba, vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta, sukari na chumvi vinachangia katika kuleta magonjwa sugu kama vile kisukari, maradhi ya moyo na kensa za aina mbalimbali, magonjwa ambayo yanasababisha vifo kwa asilimia 60 duniani kote.
Timoth Armstrong Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa Sugu na Ustawi wa Afya cha WHO amesema kwamba, unene wa kupindukia kwa watoto unaongezeka duniani. Kiwango cha ongezeko hilo katika nchi zilizoendelea ni kikubwa zaidi kwa sababu ya mabadiliko ya kasi ya lishe pamoja na jinsi mwili unavyoshughulishwa.
Yafaa kujua kuwa, tangu mwaka 1980, unene wa kupindukiwa umeongezeka mara dufu kwa watu wazima na mara tatu kwa watoto. Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa, watoto milioni 42 wenye umri wa chini ya miaka mitano wana uzito uliozidi, huku milioni 35 kati yao ni wale wanaoishi katika nchi zilizoendelea kiuchumi. Shirika hilo limeshauri kwamba, inabidi wazazi wapunguze kuwaachia watoto wao kuangalia televisheni, na mashuleni na katika sehemu za michezo za watoto kusiwe na vyakula holela na vinywaji vyenye sukari nyingi.

3 comments:

BabyAmore said...

kwa unene huo ni hatari.

NJE YA MADA SAMAHANI MAMY.

JAMANI KUNA WATU WANAKOROMA SANA, MPAKA HATA KULALA NAYE UNAJIULIZA MARA MBILIMBILI. NA WAKATI MWINGINE HATA MTU UNAONA HAYA KULALA NJE YA KWAKO.

TAFADHALI MAMY KUNA DAWA YA KUZUIWIA KUKOROMA?

asante.

Shally's Med Corner said...

BabyAmore nakubaliana na wewe kukoroma ni tatizo kubwa, na njia za kuzuia kukuroma zipo, lakini tafadhali niruhusu nilizungumzie suala hilo katika blog hivi karibuni ili watu wote wafaidike.

tweety said...

yani utakuwa umetuokoa wengi, hata mimi nina tatazo hili mpaka huona aibu kulala na mtu ambaye sijamzowea.