Wednesday, May 12, 2010

Kuchoka wakati wa ujauzito na namna ya kujiepusha

Wapenzi wadau natumaini hamjambo! kumekuwa na baadhi ya wadau wanaoniandikia na kuomba ushauri mbalimbali kutokana na matatizo waliyonayo. Nawashukuru sana kwa kuwa wanafuatilia yale yanayojiri katika blogi hii na kupata ingawa machache kuhusiana na afya zetu. Pia nawashukuru kwa kuniwezesha nami kuzungumzia mada mbalimbali kutokana na maswali yenu munayoyauliza. Kwa wale wenye maswali na matatizo mbalimbali tafadhali sana niandikieni kwa kupitia email yangu ambayo ni sthugs4j@gmail.com. Kwani wale wanaoandika maswali yao katika sehemu ya maoni, baadhi ya wakati huwa siyaoni katika muda unaotakiwa na hivyo hunifanya nichelewe kuwajibu. Wote mnashukuriwa. Leo tutazungumzia suala la kujihisi uchovu wakati wa ujauzito ambalo limeulizwa na mmoja wa wadau wanaofuatilia kwa karibu kona ya afya nami nalijibu swali lake kama ifuatavyo.

Wanawake wengi kwa kawaida huwa wanahisi uchovu wakati wa ujauzito. Uchovu, kulegea mwili na kuishiwa na nguvu ni jambo la kawaida katika kipindi hicho. Hii ni kwa sababu mwili katika kipindi hiki unatumia nguvu za kiada ili kuunda kiumbe kipya. Pia wakati huu mwili hutengeneza damu kwa wingi zaidi ili kufikisha chembechembe za chakula kwa mtoto, suala ambalo huufanya mwili ufanye kazi ya ziada na hata viungo vingine muhimu kama vile moyo na vinginevyo. Uzito wa mtoto nao unaoongezeka katika mwili wa mama mjamzito siku baada ya siku, ni sababu nyingine inayomfanya mama mjamzito ajihisi kuchoka. Kuchoka au kiushiwa na nguvu ni tatizo la kawaida hasa katika miezi mitatu ya mwanzo ya mimba. Katika miezi hiyo ya mwanzo ya mimba tatizo hilo husababishwa na mabadiliko ya homoni za mimba mwilini hasa progestrogen na wakati mwingine hali hiyo huongezwa na kichefuchefu na kutapika. Hali hiyo ya mchoko inatarajiwa kuisha inapoingia miezi mitatu ya pili ya mimba. Lakini pia kuna wengine ambao hali hiyo ya kuchoka huendelea nayo hadi wakati wa kujifungua. Kushindwa kulala vizuri kutokana na kwenda mara kwa mara msalani, au kukosa uzingizi kutokana na ongezeko la ukubwa wa tumbo mwishoni mwa ujauzito, ni miongoni mwa masuala ambayo humfanya mama mjazito ajisikie mchovu na akose nguvu siku nzima.
Vilevile mabadiliko ya kifizikia na kisaikolojia ya wakati wa ujauzito humfanya mama mjamzito awe na morali ya chini na kuhisi uchovu wa kimwili na hata kiakili. Sababu nyinginezo zinaweza kutokana na kazi mbalimbali anazofanya mama huyo au pia ukosefu wa lishe inayofaa na ya kutosha kwa ajili ya mwili wake, ambao unahitajia nguvu ya ziada hasa kwa ajili ya uumbaji wa ukamilifu wa mtoto aliye tumboni.
La muhimu analoshauriwa mama mjamzito ni kutoogopa na kutotishwa na hali hiyo, kwani inatokana na baadhi ya mabadiliko yanayotokea katika mwili wake. La muhimu ni mama mjamzito kufuata ushauri unaotakiwa ili kukabilina na hali hiyo.
Zifuatazo ni njia za kukabiliana na uchovu wakati wa ujauzito.
• Kwanza kabisa mama mjamzito anatakiwa ale vyema. Mama mjamzito anatakiwa ale chakula bora na kamili, chenye kalori 300 au 500 za ziada ikilinganishwa na mtu asiye mjamzito kwa siku. Lakini awe mwangalifu na ni bora akigawe chakula chake katika sehemu ndogo ndogo 5 au 6 (suala hili tumelizunguzia kwa undani katika makala iliyopita ya kiungulia wakati wa ujauzito, tafadhali pitia makala hizo). Anaweza akawa akibeba matunda na mboga mboga kama asusa (snacks) kwa ajili ya kula kila anapohisi njaa popote pale awapo. Lakini ni bora ajiepushe na vyakula vyenye sukari nyingi na caffeine, kwani vyakula hivyo huyeyuka haraka mwilini na kumfanya ahisi njaa mapema.
• Mama mjamzito ahakikishe kuwa hana upungufu wa damu. Na kama anao basi atumie dawa za kuongeza damu zinazotolewa na madaktari, au ale vyakula vinavyoongeza damu. Hii ni kwa sababu ukosefu wa madini ya chuma mwilini unaosababisha ukosefu wa damu, ni miongoni mwa sababu zinazomfanya mama mjamzito ahisi kuchoka. Mtu mwenye ukosefu wa damu (Anemia) huhisi kubanwa na pumzi, ongezeko la mapigo ya moyo, udhaifu, kupauka na kizunguzungu. Onana na daktari iwapo una dalili kama hizo.



• Mama wajawazito wanashauri kujipumzisha nyakati za mchana. Ni bora mama mjamzito apumzike kwa kadri anavyoweza wakati wa mchana, baada ya chakula cha mchana au hata kabla ya nyakati za magharibi. Ikiwa unafanya kazi, basi pumzika mara kwa mara japo kwa muda mfupi ili kufanya mwili upate nguvu.
• Mama wajawazito wanashauriwa kujitahidi kulala mapema, hasa kama ikiwa inakubidi uamke mara kadhaa usiku kutokana na sababu mbalimbali, kama vile kwenda msalani, kula au kutokana na maumivu.
• Kufanya mzoeni husaidia kupunguza uchovu na kuna faida kemkem wakati wa ujauzito. Kahusiana na suala hilo soma makala zilizotangulia.
• Mama mjamzito anatakiwa anywe maji ya kutosha. Ukosefu wa maji mwilini huchangia kumfanya mama mjamzito ahisi uchovu.
• Usifanye kazi nyingi kutwa nzima, na kama inawezekana ni bora usaidiwe kazi hizo hasa za nyumbani na watu wengine katika familia kama vile watoto, mume ndugu, jamaa na marafiki.
• Usikilize mwili wako. Pale unaposikia njaa basi kula na pale unapojisikia uchovu jitahidi upumzike.
• Pata ushauri wa daktari iwapo unahisi uchovu wa kupindukia au unachoka kila mara, ili uwe na uhakika kuwa hakuna tatizo au hatari inayoweza kuhatarisha maisha yako na ya mtoto.

40 comments:

Anonymous said...

NASHUKURU SANA KWA KUWEZA KUJIBU SWALI LANGU KWA KIREFU NDUGU. UMENIFANYA NISIWE NA SWALI TENA KWA WAKATI HUU. PIA WALE AMBAO HAWAJABEBA MIMBA NA WALIO NA UJAUZITO,UMEWASAIDIA VYA KUTOSHA. WADAU FUATELIENI USHAURI HUO. by merina.

Shally's Med Corner said...

Usijali Merina, nami nafurahi kwa kuweza kujibu swali lako.Tuko pamoja.

Anonymous said...

Yani nimefurahia sana hii mada mana na mimi nina ujauzito mkubwa kidogo.
Ila bado ina swali naomba unisaidie...eti ni kweli si vizuri kwa mama mjamzito kulala chali?

Mdau.

Shally's Med Corner said...

Si vuzuri kwa mama mjamzito kulala chali kwa kuwa, kutokana na tumbo kuwa kubwa, anapolala chali tumbo hubana mishipa ya damu ambayo inapeleka damu sehemu ya chini ya moyo wako. hivyo huweza kukufanya uhisi kizunguzungu. Pia unaweza kuhisi presha yako imeshuka mara moja. Kuna baadhi wanasema kulala chali pia huweza kuleta matatizo kwa mtoto aliye tumboni. kama umelala chali na ukajisikia vibaya, ni bora haraka ulala kwa ubavu. Hata hivyo mama mjamzito anashauri kulala kwa vyovyote vile ajisikiavyo comfortable.

Anonymous said...

nje ya mada. chai ya kijani inapatikana katika maduka yepi hapa jijini dar? thxs

Anonymous said...

Mimi ninamba ya miezi mnee sasa sihi kuchoka,silali mchanammda wangu wa kulala ni sa tano usiku au sa sita.je ntamsababishia mtoto matatizo?yani siwezi kalala mchana kabisa,na nafanya kazi zote mwenyewe.

Anonymous said...

Mimi ninamba ya miezi mnee sasa sichoka,silali mchana mmda wangu wa kulala ni sa tano usiku au sa sita.je ntamsababishia mtoto matatizo?yani siwezi kalala mchana kabisa,na nafanya kazi zote mwenyewe.

Unknown said...

NAOMBA KUULIZA MM NI MJAMZITO MIMBA YA MIEZI MIWILI NI SAWA MJAMZITO KULA CHIPS?

Anonymous said...

sababu zipi labda ungezifafanua zinazosababisha usipate mapumziko kwa wakati unaotakiwa, ili unapopatiwa jibu mtoa jibu awe amekuelewa vzr

Anonymous said...

Ninaujauzito wa miezi 2 mate yangu yamekuwa nimachungu sana na nimekuwa najitahidi kula matunda ila niyafanye yawe normal lakini inakuwa ni kwa kipindi kifupi tu nisaidie nifanye nn?

giftally said...

asante mtoa majibu hata mimi nimeelewa nina mimba ya miez miwili ninadamu 10.3 nimeenda kituo ch hudum cha afya na sijapatiwa dawa za aina yoyote nimeelewa hapo nitumie mboga mboga n matunda je nimatund gani yanaongeza damu mwilini? naomba nisaidiwe

Unknown said...

Yeaa bt kiasi usile sana cz viazi vina gas

Unknown said...

Hizo ni mabadiliko ya homoni ...usijali dear utakuwa sawa

Unknown said...

Utajuaje kama una mimba ya mapacha ?ikiwa mimba bado no ndogo

Kadada said...

Nashindwa kupost inajifuta

Unknown said...

Dada mm ni mjamzito wa miez 9 karibia kujifungua ilaa nahic maumiv kwa mbali chin ya tumbo na nachoka sana had I najihic kuumwa u.t.I kwani naenda choon Mara kwa Mara nishaur hii ni halo yakawaida kweli au nikapime nn

Unknown said...

mimba ina miezi 8 sasa ila tumbo linauma sana upande wa kushoto hii ni tatizo gani

Unknown said...

Asante sana nimesoma na nimeelewa Vinci nilivyo kua sivijui asante ni sana imla swali langu ni dogo tu clinic kwa mama mjamzito kwa awali kabisa inatakiwa kuanza miezi mingapi au wiki ngapi?

Unknown said...

Ahsante kwa ushauri wako

Unknown said...

Swala la Tania pia mama wengi wanapo kuwa na mimba tabis wanakuwa wasumbufuuu

Unknown said...

Wiki kumi na mbili

Unknown said...

Wiki kumi na mbili

sandra said...

Mimi ni mgonjwa wa kisukari na nina mimba ya wiki 2 na nilipata ya kwanza iliharibika sababu ya sukar je nifanyaje isiharibike hii

Unknown said...

Woow nimejifunza kitu kikubwa nimejikuta nafalijika sana nina ujauzito wa mwez miwili ila nachoka sana kuna mda sitamani hata kuongea lakini kwasasa najua ni hali ya kawaida

Unknown said...

Nina mimba ya miez miwili ila nackia uchov sana na saa ingine nikijisafisha sehem za Siri vitone vidogo vya damu vinakuwepo na tumbo linaniuma upande wa kulia, na je ni sawa kulala upande wwte kwass ambpo mimba bdo haijawakubwa

Unknown said...

Nina mimba ya miezi miwili lakini kitovuni kuna mda naumia kama panavuta ni tatizo gani linaweza kuwa?

Unknown said...

Nashukru nami nauliza eti nini kinasababisha hadi nahisi uchovu?(mimba tangu miezj9)

Unknown said...

Nashukuru kwa elimu nzuri

Unknown said...

Ahsante kwa somo

Unknown said...

Safi sana

Unknown said...

Na nikitu gani kinasababisha nyonga kukaza nakuuma na wakati mwingine kushindwa kutembea ilihali mazoezi unafanya unapumzika kwa wakati, nakaribia kujifungua lakini Hilo tatizo linanitesa sana na uke kuuma na kupata vichomi

Unknown said...

Kuchokaa kwa mwanaume pindi mke wake anaujauzito hiii Hali inakuwje

Anonymous said...

Yani hilo ndo linalonitesa mm jaman nalegea mwili mzima😢😢😢😢

Anonymous said...

Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159

Anonymous said...

Tunaahukuruu sanaaumetusaidia pakubwaaaa

Anonymous said...

Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* bahati nzuri
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159

Anonymous said...

Kuchoka Sana kupita kiasa kwa miezi mitatu ya mwanzo hii inaisha lini

Anonymous said...

Nashukulu kwa ushaili wako mimi Nina mimba ya miezi minne lakini nakuwa nasikia maumivu makali chini ya kitovu na juu ya kitovu na nilienda hospital nikapima vipimo vyote ila nilimbiw Sina tatizo lolote nishauli nifanye nini ili miweze kuwa sawa

Anonymous said...

Asante dn

Anonymous said...

Mm mkwngu anamimba ya mwezi moja lkini anachoka sana name mwenyew mailiwote unakosa nguvu pia