Sunday, May 16, 2010

Kupewa watoto sukari kabla ya chanjo kunapunguza maumivu


Watafiti wa Canada wamesema kuwa, kuwapa watoto sukari kabla ya kupewa chanjo kunapunguza maumivu. Watafiti wa Chuo Kikuu cha Toronto wamesema kwamba watoto wachanga wakipewa matone machache ya maji ya sukari, kabla ya chanjo hawatolia au watapunguza kulia. Hayo yamesemwa baada ya watoto 1,000 wachanga kupewa maji ya glukosi kabla ya kupigwa sindano na kupunguza kulia kwa asilimia 20. Utafiti huo umechapishwa katika jarida la Mafanikio ya Magonjwa ya watoto na umetokana na matokeo ya majaribio 14 yaliyofanywa kuhusiana na suala hilo. DaktaArme Ohlsson aliyeongoza timu ya utafiti huo amesema kwamba umefanywa kwa watoto wasiozidi mwaka mmoja. Pia watatifi hao wamesema kwamba, matone machache tu au nusu kijiko cha maji ya glukosi au sackrosi pia hupunguza muda wa mtoto kulia. Pia wamewashauri maafisa wa afya wawape watoto sakrosi na glukosi kabla ya kuwapatia chanjo. Wamesema kwa kuwa vyakula vitamu vina uwezo wa kupunguza maumivu ndio sababu watoto wanapopewa glukosi kabla ya chanzo huwa hawalii.

6 comments:

Disminder orig baby said...

asante sana.
ni lazima iwe sukari au hata asali ni sawa?

Shally's Med Corner said...

Mhh, tweety utafiti umesema glukosi au sakrosi ya maji, lakini nafikiri ukimpa mwanao nusu kijiko cha asali kabla ya kupewa sindano ya chanjo iwapo tu huko hospitali hatopewa hiyo glukosi na sakrosi, nafikiri inaweza kumsaidia.

Paul Akwilini said...

Asante kwa kutuelimisha nitamshauri mke wangu afanye hivyo wakati wa kujifungua. lkn je! mbona inasemekana mtoto wa chini ya mwaka 1 si vizuri akipewa sukari? ni sawa au sio sawa? by Mr.merina

Anonymous said...

Hata mimi naswali...nasikia mtoto hatakiwi kupewa kitu chochote hata maji ya kunywa mpaka afikishe miezi ya kuanzishia chakula.
Sasa inakuwaje apewe glucose? si makosa?

Mdau

Shally's Med Corner said...

Wadau, ni kweli ni bora mtoto anyonyeshwe tu kwa maziwa ya mama hadi anapofikia miezi minne, na asipewe hata maji bali maziwa ya mama yake. Na baada ya miezi minne anaanza kupewa polepole vyakula vigumu kwa utaratibu na kwa maelekezo yanayotolewa kliniki. Ni kweli haifai hata kumpa maji mtoto au glukosi anapokuwa mchanga kwani tumbo lake ni dogo, na ni bora apewe maziwa ya mama, lakini kumpa nusu kijiko cha chai cha maji ya glukosi tena mara moja kwa siku zile tu anapotakiwa kupewa chanjo ambazo si zaidi ya mara mbili au tatu kwa kipindi hicho cha miezi minne ya kwanza hakuwezi kumuathiri mtoto, bali kama uchunguzi unavyosema kutampunguzia maumivu. Mr.Merina.. sio mtoto wa chini ya mwaka mmoja hatakiwa kupewa vyakula vinginevyo ikiwemo glukosi, bali ni mtoto wa chini ya miezi minne. kuanzia miezi minne mtoto tayari anatakiwa aanze kupewa vyakula vigumu kidogo kidogo.

Unknown said...

Shukrani dear.
Ni kweli kabisa maneno yako. Lakini inatokea mama wengine wana matatizo, au amejifungua kwa operation na alichomwa nusukaputi, amechelewa kuamka, mtoto lazima atapewa glucose.
Asali nimesoma katika vitabu vya dini inaruhusiwa kwa kesi kama hizi zisizozuilika kwani haina mchanganyiko wa chemicals. Lakini iwe asali kweli siyo hizo shira zinazouzwa mitaani.
Na kama utatumia asali ni vizuri ukaichemsha na maji, ukayapoza ndiyo ukampa mtoto.

Asali pia inasaidia mtoto kupata choo, kama kuna hili tatizo. Mama wengine maziwa yao ni mazito sana.
Hii imenitokea mwenyewe, na mwanangu alipewa maji ya asali pale ilipotokea tu. Haipiti muda utaona habari yako.

Ni vizuri tukifuata ushauri wa wataalamu wetu.