Friday, May 7, 2010

Kweli lishe bora inaongeza umri…. Afa akiwa na miaka 114!


Mwanamke wa Kijapan aliyevunja rikodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa mtu mzee zaidi duniani amefariki dunia siku kadhaa zilizopita, akiwa na umri wa miaka 114 na siku 357. Mwanamke huyo aitwaye Kama Chinen alikuwa akiishi katika kisiwa cha Okinawa na alifariki dunia Mei 2, ambapo aliishi na kushuhudia karne tatu!. Inasemekana kuwa bibi huyo aliishi muda mrefu kwa kuwa lishe yake ilikuwa chai ya kijani, supu ya miso, mboga mboga, wali na samaki freshi. Bi. Chinen sio makazi pekee wa eneo hilo la Japan aliyeishi muda mrefu, kwani ripoti zinasema kuwa watu wengi wanaoishi eneo hilo huishi maisha marefu na ni kutokana na lishe yao. Japan ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na kiwango kirefu zaidi cha maisha ya watu (Highest Life Expactancy) huku Okinawa ukiwa mji ulio na watu wengi wenye umri mrefu, suala ambalo linatokana na lishe bora na hali ya hewa ya kisiwa hicho.
Kwa mujibu wa utafiti, mji wa Okinawa una kiasi kidogo sana cha watu wenye magonjwa ya kensa, na hiyo inatokana na watu kula vyakula vyenye mafuta kidogo, kalori chache, ufumwele kwa wingi na mboga mboga na matunda kwa kiasi kikubwa. Pia suala lingine ni kujishughulisha kwao na wala sio kukaa tu.

3 comments:

Disminder orig baby said...

Mungu amrehemu. umri wetu sisi hiyo ni ndoto ya mchana huku unatembea, halafu mara unagongwa chali.

Anonymous said...

chai ya kijani inapatikana maduka yepi kwa hapa jijini dar?

Shally's Med Corner said...

mdau, pole mie siko dar na sina utaalamu wa maduka ya huko, lakini jaribu kuulizia katika maduka ya vyakula vya kichina, kwani hao huwa hawakosi.