Saturday, September 18, 2010

Huraa! Maambukizo mapya ya Ukimwi yapungua Afrika!


Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba nchi zilizoko chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika zinaongoza kwa kupungua maambukizo mapya ya virusi vya Ukimwi. Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulia masuala ya Ukimwi (UNAids) kimesema kuwa nchi 22 ambazo ziko katika eneo hilo la chini ya Jangwa la Sahara lenye maambukizo makubwa zaidi ya Ukimwi duniani zimeshuhudia kupungua maambukizo ya ugonjwa huo kwa asilimia 25!. Kupungua maambukizo hayo kumetokana na watu kuelewe vizuri na kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo pamoja na kutumiwa vyema njia za kujikinga. Hata hivyo Umoja wa Mataifa umesema kwamba maambukizo mapya ya Ukimwi yameongezeka huko mashariki mwa Ulaya, katikati mwa bara Asia, na miongoni mwa wanaume mashoga katika nchi zilizoendelea. Mkurugenzi Mtendaji wa UNAids Michel Sibide amesema kwamba, dunia inapiga hatua kubwa katika kufikia utekelezwaji wa Malengo ya Sita ya Maendeleo ya Milenia (MDG6) ya kupambana na kupunguza maambukizo ya HIV/Aids hadi kufikia mwaka 2015. Shirika hilo aidha limesema kuwa, kuwa watu milioni 5.2 wanapatiwa matibabu ya Ukimwi duniani kote, suala ambalo limesaidia kuhakikisha kwamba watu wachache zaidi wanakufa kutokana na virusi vya ugonjwa huo hatari ikilinganishwa na huko nyuma.
Haya shime jamani tuendeleze kwa nguvu zote mapambano dhidi ya Ukimwi!

4 comments:

Anonymous said...

du ww kweli unajua kulala ucngizi wa pono, he c utafute m2 akusaide kuapdate blog yako. na kwa taaarifa yako hapa mambo ya maleria hayana dili, ukitaka wadau weka habari za uzazi.

kuwa mjanja ndugu, lazima uelewe mahitaji ya watu.

Anonymous said...

watu wengine sijui vipi, eti anasema mambo ya maleria hayana dili malaria inaua kushinda ukwimi shauri yako... mwacheni Dokta wa watu inaonyesha yuko busy anaongeza ujuzi ili atufaidishe zaidi, eti atafute mtu amsaidie! hapa ni elimu kwenda mbele unafikiri ni blog ya mitindo lol.

Shally's Med Corner said...

mie nabaki kucheka tu nisemeje,? blog naipenda lakini nimetingwa jamani!!!!!!!, lakini nakubali kukosolewa na nitajitahidi kujirekebisha ingawa kweli ningekuwa na mtu wa kushirikiana naye ningefurahi. Nakaribisha mapendekezo inabidi atleast mtu awe na elimu ya afya au tiba katika uwanja wowote na pia aijue vyema lugha ya kiswahili na kiingereza hasa maneno ya kitiba. Nakaribisha sana ushirikiano. nitumieni mapendekezo katika email yangu. ingawa kumbuka kuwa,hakuna malipo wala posho ni kujitolea tu katika kuifundisha jamii. Tushirikiane jamani.

Anonymous said...

Yani wewe ndio husomeki kabisa naomba nikwambie Malaria inaua zaidi tena kwa kipindi kidogo sana na pengine hata dk 5 ni nyingi tunakubadili jina MAREHEMU