Monday, September 6, 2010

Wataalamu karibu watakugundua dawa nyingine ya kutibu Malaria


Matokeo ya utafiti wa kimataifa yanaonyesha kwamba wanasayansi karibu watafanikiwa kutengenza dawa yenye athari zaidi ya kutibu ugonjwa wenye kuleta maafa mengi wa Malaria. Dawa hiyo inayoitwa "NITD609" ambavyo inatokana na mada ya 'spinoindolones' imeanza kutengenezwa kwa jitihada mbalimbali za wanasayansi wa Marekani, Singapore, Switzerland, Thailand na Uingereza. Wanasayansi hao wanasema kwamba, dawa hiyo ambayo ni ya kumeza inatofautiana na dawa nyinginezo za Malaria zilizopo madukani kwa kuponya ugonjwa huo haraka, kutokuwa na madhara kwa mtumiaji na kuweza kutibu Malaria kwa kutumiwa dozi moja tu.
Utafiti bado unaendelea kuhusiana na majaribio ya dawa hiyo na kwamba dawa hiyo imeonyesha mafanikio mazuri katika kutibu Malaria baada ya kujaribiwa kwa panya watano waliokuwa wagonjwa bila kuwa na madhara yoyote.
Wataalamu wanasema pia kwamba dawa hiyo ya NITD609 inatofautiana sana na dawa ziliopo za Malaria kwa umbo na kwa kikemia na kwamba ingawa dawa zilizopo zinaweza kutibu ugonjwa huo lakini zimeshindwa kufikia matarajio yanayotakiwa. Wataalamu sasa wanasubiri kuijaribu dawa hiyo kwa binadamu, suala ambalo litaanza baadaye mwakani.
Ingawa sote tunajua lakini si vibaya kukumbusha hapa kuwa watu karibu milioni 500 huugua ugonjwa wa Malaria kila mwaka duniani, ambapo vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo ni karibu milioni moja huku watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano ndio wanaoshambuliwa zaidi na Malaria. Ugonjwa huo umekuwa ukisababisha vifo na matatizo mengi katika nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika kuliko maeneo mengineyo duniani.

7 comments:

Anonymous said...

okay, maleria haikubaliki ni sawa hilo tunajua.

plz ndugu tuendelee na mada za uzazi banaa, tusaidei jamani na sisi tuitwe mama. dozi nilimaliza na nimeona tena cku zangu tarehe ileille 1/09. au jamaa mbegu dhaifu? mana sielewi ujue, inabidi nikacheki vipimo. au vp eee?

Gg

Anonymous said...

dada Gg pole sana. jaribuni ku- sex kuanzia tarehe 12 mwezi huu hadi tarehe 17. mkifanikiwa utajifungua tarehe 8june 2011. by P.A.

Shally's Med Corner said...

Dada G,
Suala la kubeba mimba linaathiriwa na sababu mbalimbali, sio kwamba tu kama mwanamke anapata damu yake ya mwezi katika siku zinazotakiwa, anazijua siku zake za Ovulation basi lazima apate mimba iwapo akifanya tendo la ndoa katika siku zinazotakiwa. Kidogo fanya subira endelea na mwendo huo huo mungu atakujalia nawe uwe mama. lakini pia Ninachotaka kusema hapa ni kuwa hiyo ndio hali ya kawaida inayotakiwa kuwa, lakini iwapo hilo halijatokea pengine kunaweza kuwepo na matatizo mengine. Kama vile mwanamume pia anatakiwa kuhakikishwa kwamba ana mbegu, za kutosha na zenye nguvu na mwanamke kutokuwa na matatizo mengineyo. basi ili kukusaidia suala hilo nitazungumzia matatizo yanayosababisha mtu asishike mimba. Mdau P.A ahsante kwa kuchangia, hilo pia limo...du! itabidi kweli nichangamke au nifikirie kubinafsisha blogi... lol!

Disminder orig baby said...

Dada G,

pia tention inaweza sababisha ukachelewa kupata mimba, unatakiwa uwe relaxed, yaani mind yako iwe free from those filings.
asilimia kubwa wanapata mimba kipindi ambacho hata hakuwa na ile tension, ukifanya mapenzi kwa kuweka nia, inawezekana pia ikakupotezea point za kufika golini, relax mind darling na Mungu atakujalia.

hii nilipewa na doc wangu.

Anonymous said...

nashukuru jamani, ushauri wote naufata.kiukweli huwa nafika kileleni kila mchezo, yani huwa najiachia sana tu. naona nikajicheki kwa doc. then nitawajulisheni wats problem. tuko pamoja wadau. mbarikiwe

Gg

Anonymous said...

Dr kanyas mtaalamu wa tiba asili anazo dawa kwa ajili ya nguvu za kiume na kurefusha uume na kunenepesha uume ...dawa zake ni mitishamba asili hazina madhara ...anatibu UTI NA PID SUGU anatibu UGUMBA.. ..MAUMIVU makali WAKAT WA HEDHI NA CHINI YA KITOVU.afigo..moyo..presha ..kisukari ..mtafute docta kupitia 0764839091

Anonymous said...

Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159