Wednesday, September 8, 2010

Mambo ya kuzingatia iwapo unataka kushika mimba


Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu asishike mimba. Sababu hizo zinaweza zikawa zinamhusu mwanamke, mwanamume au wakati mwingine kutojulikana kabisa hali hiyo imesababishwa na nini. Wataalamu wanasema kwamba kwa miaka 20 iliyopita matatizo yanayohusu kushindwa kuzaa yameongezeka kwa kiwango kikubwa na asilimia 25 ya watu wanaotaka kubeba mimba na kuzaa mtoto wanakabiliwa na tatizo hilo. Ni kweli kuwa kwa kawaida watu wengi hubeba mimba na kujaaliwa mtoto pale tu wanapofanya tendo la ndoa. Lakini jambo hilo halitokeo kwa watu wote na ingawa kwa baadhi ya watu kila kitu huonekana kwenda sawa lakini pia hushindindwa kubeba mimba. Utafiti unaonyesha kwamba katika kila familia au 'couples' 5 zinazojamiiana katika wakati muafaka wa ovulation ni moja tu ndio hufanikiwa kupata mtoto, huku karibu wanawake 9 kati ya 10 wakifanikiwa kushika mimba baada ya kujaribu kutafuta mtoto kwa mwaka mmoja mzima bila kuzuia mimba. Hivyo basi nawaomba wale ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kufuata maelekezo ili waweze kushika mimba lakini hawakufanikiwa, wasife moyo kwani ipo siku jitihada zao hizo zitazaa matunda.
Mambo ya kuzingatia iwapo unataka kushika mimba…
• Kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa kabla ya yote unamona dokta wako au unakwenda hospitalini na kufanyiwa vipimo ili kujua kama afya yako iko salama au la kwa ajili ya kushika mimba. Baadhi ya vipimo vinavyoshauriwa kufanywa ni pamoja na
1. General examination au uchunguzi wa jumla.
2. Kipimo cha kensa au Pap smear.
3. Kipimo cha magonjwa ya zinaa (STD) kama vile Chlamydia ambao wanaweza kuathiri uwezo wako wa kushika mimba.
4. Kipimo cha damu cha kuangalia kama una upungufu wa damu, Rh na kinga yako ya mwili dhidi ya ugonjwa wa Rubella.
5. Kipimo cha mkojo cha kuchunguza iwapo una ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa wa kisukari huweza kumzuia mtu asishike mimba hata iwapo mzunguko wake wa mwezi uko sawa, anapata Ovulation na kidhahiri anaonekana hana tatizo lolote.
6. Kama una paka nyumbani au unakula sana nyuma (red meat) pengine si vibaya pia kupima kipimo cha Toxopmasmosis infection.
7. Kuyajua na kuzingatia baadhi ya mambo yanayoathiri kushika mimba ambayo ni pamoja na:-
• Ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia pia huathiri homoni mwiilini.
• Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo 'stress' huweza pia kauthairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.
• Kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanamme baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba (nitazungumzia vyakula vinavyosaidia kushika mimba baadaye)
• Sigara, marijuana na pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba. Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara. Mwanamume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha mbegu za kiume za mwanamme.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomsaidia mwanamke kushika mimba:
• Anza kutumia vidonge vya Folic Acid, vidonge hivyo mbali ya faida nyinginezo humkinga mtoto atakayezaliwa na magonjwa ya ubongo. (Neural Tube Defect) kama vile Spinal Bifida na mengineyo. Dozi ni kwa uchache miligramu 0.4 za Folic acid kwa siku, miezi mitatu kabla ya kuanza hata kutafuta mtoto.
• Endelea tu na tendo la ndoa bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache kabla ya Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanamume aweze kuboreshe na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo, Usikimbie chooni au bafuni baada tu ya kukutana kimwili na mwenzio. Kulala kwa dakika kadhaa baada ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.
• Jiepushe kunywa kahawa na binywaji vinginevyo venye caffeine. Waataalamu wanasema caffeine huweza kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.
• Jiepushe na kutumia dawa za aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada ya kushauriana na daktari.
• Usitumie baadhi ya vitu vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji yake. Vitu hivi ni kama spray mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri. Mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na mate. Vitu kama hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume.
• Hakisha mwenzi wako hafanyi kazi au hawi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu za kiume au kutungwa mimba. Kufanya kazi kwenye mazingira ya joto kali sana kama vile mwanaume wanaofanya kazi kwenye matanuri ya kupika mikate, viwanda vya mafuta na miale hatari baadhi ya wakati huwa na matatizo ya kutozaa. Hivyo kabla mwanamke hajaanza kujilaumu kwa nini hashiki mimba, mwanamme wake pia anapaswa kufanyiwa uchunguzi kamili kuhusiana na suala hilo. Pengine ni suala ambalo wengi hatulijui kwamba katika tiba iwapo mke na mume au mtu na mwenzi wake wana tatizo la kutopata mtoto, wawili hao kwa pamoja hupaswa hufanyiwa vipimo na wala sio mwanamke mwenyewe. Hivyo iwapo unashindwa kushika mimba, hakikisha pia mwenzi wako hana tatizo pia. Wanaume pia kama walivyo wanawake hukabiliwa na matatizo mengi tu yanayosababisha familia kukosa watoto. Matatizo kama vile upungufu wa mbegu za kiume, uchache wa mbegu, kutokuwa na kasi mbegu na mengineyo ni miongoni mwa matatizo kibao ambayo mwanamume anaweza kuwa nayo na kukosa mtoto. Hivyo tabia ya kuwatizama wanawake kwa jicho la lawama katika jamii na kuwanyooshe kidole pale mimba inaposhindikana kushika ni kinyume cha ukweli wa kitiba na uhalisia.
• Usichoke kufuata mzunguko wako wa Ovulation na kufanya tendo la ndoa katika wakati ambao mwili wako (ewe mwamamke) uko katika siku za kuweza kushika mimba.

48 comments:

Anonymous said...

okay, tuko pamoja ndugu, mada nzuri sana. mm binafsi nashukuru sana. wat i decide is to go to meet doctor ASAP, and wen i cam back i will let ol of u knw wats then. continue.....

Gg

Shally's Med Corner said...

Okay dada Gg, nakutakia kila la kheri na Mungu ajaalie tatizo lako litatuke.Tuko pamoja :) usijali!

Anonymous said...

thanks a lot dk shell kwa msaada wako ktk kutupa ufahamu juu a kushika mimbaa nachotaka kujua ni kwamba mie ni mmoja kati ya watu wanaosaka mtoto so kitu nachotaka kujua hapa tatizo langu ni nini napata siku zangu kama kawaida lakini sinasi na tumeenda kupima mimi mume wangu mie ultral sound na mwenzangu kipimo cha speaci man na majibu yetu wote yametoka ya kwangu yameandikwa ultras promblem na mume wangu yake yameandikwa spem thin je kwa majibu hayo tunaweza kushika mimba

Shally's Med Corner said...

Mdau, pole sana kwa matatizo mlio nayo ingawa kuhusu wewe mwenyewe sijaelewe unakusudia nini unaposema umefanyiwa ultrasound majibu yako yameandika una ultras problem. Lakini kuhusu mumeo low thin sperm inamaanisha low sperm count ambayo maana yake ni kwamba kiasi cha mbegu za kiume cha mumeo hakitoshi au ni kidogo na hilo ni miongoni mwa matatizo ambayo husababisha mimba ishindwe kushika. Suala hilo huweza kusababishwa na matatizo au hali mbalimbali. Kwa wanaume suluhisho la tatizo hilo kuhusiana na kupata mtoto inategemea sababu iliyosababisha sperm thin na mara nyingi hutumia njia ya IVF ili kusaidia kupata mimba. Lakini ndugu mdau kwa kuwa pia wewe umesema kwamba ultrasound imeonyesha una matatizo basi inabidi nawe utibiwe tatizo lako ili muweze kupata mtoto.

Anonymous said...

dk asante sana kwa uelimishaji wako ila mimi ni mwanaume nemeoa sasa nina miaka mitatu ya ndoa yangu hatujafanikiwa kupata mtoto sasa imefikia wakati tukashauriana twende hospitali kwa ajili ya vipimo, na tumeanda lakini majibu yametoka ya kwangu na tumpango wa kurudi tena hospitali tukamuone dk ili atupe majibu,lakini bahati nzuri katika pitiapitia yangu blogs nikakutana na blog hii nzuri kabisa anayotufundisha mambo ya afya asante sana dk,vipimo vyangu,GROSS: Appearance-cream white,Consistency-thin,Volume-1.5 ml ph 8.0 niSPERM MORTALITY rapid progression 40%,slow progression 20%,non progressin10%,count/ml:85 milion,naomba majibu kabla sijaenda na dk na wife wangu kucheck wote hapa nasubiri majibu ya wife ili wote tupeleke result

Anonymous said...

samahani dada hicho kifupi cha IVF ni nini maana ingenisaidia kujua ni dawa gani ingenisaidia asante

Shally's Med Corner said...

Ndugu mdau IVF au ni matibabu yanayoondoa tatizo la kutokuzaa ambapo yai na mbegu ya kiume huunganisha na kukutanisha katika maabara (laboratory). Njia hiyo hupelekea kutunga mimba nje ya mwili na embryo huhamishwa katika kizazi cha mwanamke kupitia uke na mimba huanza kukua.

Anonymous said...

asante sana kwa kunijulisha nilikuwa sifahamu je kwa hapa Tanzania ni hospitali gani inayoweza kufanya IVF maana umri unazidi kukimbia tumesaka mtoto mpaka tunasubiri rehema za Mungu kwetu asante

Shally's Med Corner said...

Pole sana mdau, usife moyo matatizo mengi ya uzazi yanaweza kutatuliwa kwa urahisi hasa kwa kuzingatia maendeleo ya teklojia tuliyonayo hivi sasa, mimi siko Tanzania na kweli sina ufahamu sana kuhusiana na hospitali za huko. Pengine ujaribu Muhimbili labda wanaweza wakawa wanafanya IVF kwani hiyo ni hospitali kubwa ya kitaifa. Nakutakia kila la kheri lakini kama una uwezo kni bora ukashuhulikie tatizo hilo nje, kwani ni rahisi sana kutatuliwa.

Anonymous said...

aasante sana dokta ubarikiwe kwa shauri mzuri nimekuelewa Mungu aibariki kazi yako ya kuelimisha jamii iendelee daima dumu

Anonymous said...

dk asante sana kwa kutupatia email yako tutawasilisha maswali yetu kupitia anuani hiyo ilaa mbana dk umenichunia kujibu swali langu mimi ni anonymous septemer 14 8:22

Anonymous said...

Hi Shally,
mbona nimekutumia mail kwenye e-mail yako binafsi tangu tar 27/10ambayo umeitoa kwa wale wanaotaka majibu mapema kwa kuchangia mada iliyopita, lakini kwa bahati mbaya hujanijibu. Tafadhali naomba unijibu kupitia e mail yangu niliyokutumia nayo.
THANKS IN ADVANCE.
STAY BLESSED.

joyce said...

Asante sana Dk. kwa mafundisho yako kwani watu wangi husumbuliwa na tatizo hilo.
swali langu ni:Je, mme na mke ambao ni HIV+ wanaweza wakafanyiwa IVF na wakamzaa mtoto ambaye hajaathirika?

Shally's Med Corner said...

wapenzi nimerudi na naahidi kuwajibu wote email zenu. Shukrani kwa kunivumilia muda mrefu ni majukumu ya maisha, kazi na kitabu nimerudi shuleni mwenzenu kuongeza ujuzi.

Anonymous said...

je nitajuaje kama ina mimba ya mtoto wa kike au wa kiume?

Unknown said...

Je ufanyaji wa mapenzi wa kila siku unaweza kuzuia upatikanaji wa mtoto?

Mrs Patrick said...

Dr asante saana kwa somo lako, nimeona umeandika kuwa kama uzito ni chin ya 50 huwez kushika mimba, na mm Nina uzito wa 47_49, na nimehangaika na mume wangu hatupat mtoto zaid ni fangas ukeni,pia naomba unishauri jinsi ya kutumia hiyo doz ya miez3 ili inisaidie niahike mimba, hospital niliambiwa sina tatizo lolote,so naomba msaada wako

Mrs Patrick said...

Naomba nielekeze jonsi ya kuitumia hiyo folic acid na je naweza kuipata katika maduka ya dawa yoyote au mpaka hospital

tintii said...

Mpezi wangu ame pata mimba lakini ipo nje ya mfuko wa uzazi na ukitoa una aababisha matamozo megime baadae mifanyeje ?

Anonymous said...

Mimi ningependa kuulizia kuhusu namna ya kukusanya nguvu hasa kusubiri siku ya ovulation. Kuna mtu nilisoma makala yake akasema kwamba hata ukifanya kila siku mapenzi haina athari na kwamba ndo mbegu mpya huzalishwa. Je ukweli ni upi?
Pia je ni vzr kusubiri kabisa ovulation day au mimba hutungwa wakat wowote wa fertility?

Anonymous said...

thanks a lot dk shell kwa msaada wako ktk kutupa ufahamu juu a kushika mimbaa nachotaka kujua ni kwamba mie ninataka ssana mtoto ila ndo hiyo mimba sipati kwa sababu ya tumbo la chango na pia ninamaumivu kwny tumbo la chini upande wa kushoto na inasababisha napata maumivu wakati wa kufanya mapenzi na mume wangu. nimesha enda hospital na kufanyiwa vipimo na gyno but they always tell me sina tatizo na viungo vyangu vipo vizuri tu! wakati mwingine nahisi ndo mana i dnt cinceive but what could be a problem? kitu kingine doctor my breats yanatowa maziwa ni mwaka wa 3 sasa ilahospital wananimbia ninahormon imbalance na sion kama dawa zao zinanisaidia wala kutuliza tatizo.

Unknown said...

Dr.nimesoma utaratibu na mashauri uliyotupa kuyafata wale tulio na matatizo ya ndoa kwenye familia zetu.lakini nyakati zengine unapata pia upande Wa mke wakati wake Wa hedhi inarukaruka na kupata ni vigumu kujua wakati rasmi Wa kufanya na kutenga siku ya kukutana na mumewe.je,hili huletwa na nini haswa Dr? (Plz Dr.naweza pata number yako ya simu?)

Unknown said...

Ahsante dr. naomba namba yako ya simu juu nina shida kibao ambazo nahitaji kukueleza binafsi. ahsante barikiwa

Unknown said...

tanzania huduma hii ya kukutanisha yai na mbegu ya kiume ktk maabara na kuhamishia ktk kizazi cha mwanamke ipo

Unknown said...

Mimi napenda kufahamu tuu kuhusu namna ya kutumia iyo folic acid, msaada wako tafadhali daktari

Unknown said...

Tunashukuru kwa ushauri wako

Unknown said...

Tunashukuru kwa ushauri wako

Afyablog said...

Asante sana Dr. kwa ushauri wako mzuri na wenye matumaini mapya kwa wale waliokosa matumaini. nina swali moja la kukuuliza. Je magonjwa kama UTI, Kaswende, Kichocho, na mengine kama hauyo yanaweza kusababisha mwanamke kushindwa kubeba mimba.

KANYAS YUSUPH said...

Dr kanyas mtaalamu wa magonjwa mbalimbali anatibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia dawa za asili na za kisuna..anasaidia kushika mimba..ugumba..upungufu wa nguvu za kiume...uchafu ukeni..uti..malaria sugu..anazo dawa za asili za kurefusha uume na kunenepesha uume..hedhi isiyo na mpangilio...maumivu makali chini ya kitovu wakati wa hedhi..mtafute docta kupitia 0764839091...dawa zake ni za kisuna na mitishamba asili

KANYAS YUSUPH said...

Dr kanyas pia anazo dawa kwa ajili ya uke uliotanuka ...uziwi na magonjwa ..kurefusha na kunenepesha uume....mabalimbali..mtafute kupitia 0764839091

Dr kanyat said...

Dr kanyas mtaalamu wa tiba asili toka tanga ..anazo dawa asili kwa ajili ya mapungufu ya nguvu za kiume ..pia anazo dawa kwa ajili ya kurefusha uume na kunenepesha uume...anatibu UGUMBA ..UTI..PID..KISUKAR..PRESHA ..FIGO...DAWA ZAKE ZOTE NI ASILI MTAFUTE KUPITIA 0764839091

Unknown said...

Mimi nilishawah kushika mimba ila ckubahatika mtoto mimba ilitoka nikasafishwa lakin baada ya hapo cjabahatika tena je nini nifanye ili niweze kufanikisha naomba msaada restynjau@gmail.com

Unknown said...
This comment has been removed by the author.
Unknown said...

Nifanyeje ili kupata dawa ya homoni balance. Maana ninahitaji mtoto

Unknown said...

Ninaomba msaada wa suluhisho la kupata mtoto, maana nimuda mrefu sasa sipati ujauzito wakati situmii njia yoyote ya uzazi wa mpango. Isipokuwa nimewahi kwenda kwa daktari wa Mama nikapiga utrasound nakuambiwa ni homoni balance. Naomba msaada tafadhari nifanyeje?

Mwafrica Mtanzania Mzalendo said...

Inakuaje mwanamke alisha zaa na mwanaume mwingine na huyu alie nae sasa pia alisha zaa na mwanamke mwingine ila sasa wawili hawa hawana mtoto walio zaa pamoja ? nini shida

Unknown said...

Mungu ndio msaada mkubwa wa yote zingatia vigezo pia usichoke
Kuomba

Unknown said...

Doctor nilizaa miaka sits iliyopita nahitaji kuzaa sasa lkn sishiki nmeenda hospital vpimo vmeonyesha nna overian cyst nimeandikiwa dawa aina ya doxacilin na azythromycin doz nmemaliza lkn tatizo bado je nifanyeje?

Unknown said...

Naomba kufahamu mm natamani kushika mimba Lkn sipat na situmii kinga yeyote hospital nimepima ni u.t.i na fangas sasa sijui ndio chanzoo

Unknown said...

Mm sijawahi kushika mimba na nimejaribu kuchunguzwa Sina tatizo naambiw nifanyeje

Unknown said...

Nashida naweza kukupat tofaut

Khadij bakari said...

Docta naweza kupata namba yako ninashida binafsi

Unknown said...

Habari dada kwa nje nchi ipi naweza pata hiyo huduma na gharama nishingapi

Anonymous said...

Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159

Anonymous said...

Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* bahati nzuri
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159

Anonymous said...

Je UTI inaweza sababisha mwanamke asipate ujauzito

Anonymous said...

Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
Anasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka mume/mkeo arejee.
*Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159

Anonymous said...

Je U.T.I inaweza kusababisha mtu asishike mimba