Sunday, May 2, 2010

Kula aina mbalimbali za matunda kuna faida zaidi kiafya



Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba watu wanaweza kukabiliana kirahisi na magonjwa mbalimbali kwa kula matunda ya aina mbalimbali na mboga mboga badala ya kuongeza idadi ya matunda na mboga mboga hizo. Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliotolewa katika Kongamano la Majaribio ya Kibiolojia huko Anahein California, baadhi ya matunda na mboga mboga yana faida kubwa ya lishe kuliko mengineyo. Uchunguzi huo umeeleza kwamba,ingawa karoti inaaminiwa kuwa ni chanzo kikubwa cha beta-carotene lakini kula viazi vitamu badala ya karoti kunaweza kuupatia mwili beta-carotene mara dufu kuliko karoti. Papai nalo lina beta-cryptoxanthin mara 15 zaidi ya machungwa. Halikadhalika mboga aina ya Kale huupatia mwili mada ya lutein/zeaxanthin mara tatu zaidi ya spinachi. Pia imeelezwa kuwa stroberi na rasberi zina ellagic asid mara tatu zaidi huku kikombe kimoja cha maji yanayotokana na mmea uotao majini wa watercress ikiwa na mada ya isothiocyanate sawa na inayopatikana katika vijiko vine vya chai vya haradali au mustard. Bi. Keith Rabdolph aliyeongeza uchunguzi huo anashauri kwamba, watu wajitahidi kujua umuhimu wa vyakula wanavyokula na kujua pia ubora na faida za matunda na mboga mboga wanazokula kwa afya ya miili yao.

4 comments:

Anonymous said...

Pole na majukumu, mimi ni mdau mzuri wa kona ya afya na nashukuru sana kwa mada zako za kutuelimisha.
Mimi ninatatizo moja...mdomo wangu unabadilika rangi na kuweka kama kovu au niite doa kama rangi ya kidonda ambacho kinaanza kupona. (Wekundu)
rangi yake ni kama mabaka yanayotoka mwilini kwa dalili za wagonjwa wa ukoma.
Kwa kweli hali hii inaninyima raha sana naomba ushauri wako au kama unajua tiba yake pls

Unknown said...

lovely, thank you

Shally's Med Corner said...

Ndugu mdau, kwanza pole kwa kuchelewa kukujibu, na pili
kuwa na mabaka katika mdomo kunaweza kusababishwa na matatizo mbalimbal.
Inaweza ikawa ukosefu wa vitamini, kulamba sana mdomo, hali ya hewa, allergy ya chakula, sigara na hata kensa. Nakushauri umuone
daktari ili akupatie vitamini zinazotakiwa, ushauri na yale yanayotakiwa kufanya. Pengine kwa kula vitamin ambayo huenda mwili wako umekosa tatizo lako likaondoka. Kuhusiana na matatizo mbalimbali ya mdomo nitaandika makala katika blogi ambayo tafadhali naomba uifuatili ili kujua zaidi.

Anonymous said...

jambojambojambojsera za matunda nilizotoa katika uchaguzi 2010,ubunge jimbo la moshi mjini zinanisumbua sana. niliahidi kupanda miti ya matunda jimboni kote watu wale matunda bure,lakini sasa nimeshindwa na mhe; ndesa pesa.
sasa wananchi wanataka matunda ni sera nzuri nifanyaje kwani utekelezaji wake unategemea madaraka.
isaac kireti, mgombea ubunge ,chama cha sau,moshi mjini.