Saturday, June 19, 2010

Kunywa maji kwa mpangilio husaidia kurahisisha utendaji wa mwili



Kila mtu anajua umuhimu wa maji katika miili yetu. Sio kwamba tu mwili wenyewe umejengwa kwa asilimia kati ya 55 na 75 za maji (kwa kutegemea unene wa mtu ambapo watu wembemba wana kiasi kikubwa cha maji mwilini kuliko wanene) bali pia mwili unahitajia maji kwa kiasi kikubwa ili kufanya kazi zake vyema.
Je? Unajua mapafu yako yanahitajia vikombe wiwili vya maji hadi vinne kila siku ili kufanikisha kwa ufanisi kazi yake ya kupumua? Na kiasi hicho huhitajika ziadi wakati wa baridi.
Je, unajua wakati unapotoka jasho kikombe kimoja cha maji hupungua mwilini mwako. Na je, unatambua kwamba iwapo utaoga wakati wa mchana kwa mara karibu tatu kwa siku ni kana kwamba umekunywa vikombe 6 vya maji?
Kunywa maji kwa kiasi cha kutosha husaidia kupunguza uwezekano wa kutokea mawe katika figo, hulainisha viungo na huzuia mafua na kusaidia kupona haraka ugonjwa huo. Vilevile kunywa maji husaidia mtu kupata choo vyema.
Maji ni hitajio la dharura kwa afya zetu, kwani asilimia 60 ya uzito wako ni maji na kila mfumo wa mwili wako hutegemea maji ili kufanya kazi zake. Ukosefu wa maji mwilini humfanya mtu akaukiwe na maji au dehydration, hali ambayo hutokea pale mtu asipokuwa na maji ya kutosha mwilini ya kuuwezesha mwili wake kufanya kazi zake za kawaida. Hata katika upungufu mdogo wa maji mwilini, wakati ambapo asilimia 1 hadi 2 ya uzito wa mwili inapopungua, huweza kumfanya mtu akose nguvu na ajisike amechoka. Miongoni mwa dalili za upungufu wa maji mwilini ni:
• Kukihi kiu sana
• Uchovu
• Kichwa kuuma
• Mdomo kukauka
• Kukosa mkojo au kiasi cha mkojo kuwa kidogo.
• Udhaifu wa misuli
• Kuhisi kizunguzungu


Ni muhimu kujua kwamba mwili hupoteza maji kila siku kwa kutokwa na jasho, iwe jasho hilo umelihisi au haukulihisi, kutoa pumzi nje (exhaling), kukojoa na harakati ya tumbo. (bowel movement). Ili mwili wako uweze kufanya kazi vizuri unahitajia kurudisha maji hayo mwilini kwa kunywa vinywaji mbalimbali na vyakula vyenye maji.
Wataalamu wengi wanakubaliana kuwa mwanadamu anahitajia kunywa vikombe 8 vya maji kwa siku, ili kufidia maji yanayopotae mwilini. Hata hivyo wengine wanashauri kwamba, wanaume wanywe vikombe 13 vya maji kwa siku na wanawake vikombe 8 vya maji, na hiyo ni kutokana na tofauti ya miili yao. Tunashauriwa kuwa badala ya kunywa maji kiholela tunywe kwa mpangilio maalum kwa siku, ili kusaidia vyema katika kazi za mwili.
 Tunashauriwa kunywa vikombe viwili vya maji asubuhi pindi tunapoamka, kwani husaidia kuamsha viungo vya ndani ya mwili.
 Tunashauri tunywe kikombe kikoja cha maji dakika 30 kabla ya mlo, kwani husaidia kupata choo vizuri.
 Tunashuariwa tunywe kikombe kimoja cha maji kabla ya kwenda kuoga, husaisia kupunguza shikizo la damu.
 Na tunashauriwa kunywa kikombe kimoja cha maji kabla ya kulala kwani kufanya hivyo huzuia shinikizo la moyo.
Basi kunywa maji kwa afya yako mdau!

10 comments:

Unknown said...

maneno kuntu. asante sana.

Anonymous said...

pole na honger na majukumu ya kutuelimisha. Mi naomba uliza swali nje ya mada hii ya maji, mimi nina hitaji kushika mimba. kwa mfano mwez huu nilianza period tarehe 17 June. Je! siku zangu za kushika mimba ni zipi? na Je nikitaka mtoto wa kike nifanyeje? naomba sana mnisaidie kwa ilo

Disminder orig baby said...

swali zuri sana anony wa 1:17PM

Tupe zaidi nasi tufaidike.
Usisahau na ile ya kukoroma jamani tumesubiri sana.

Shally's Med Corner said...

Wadau, ahsanteni sana na samahani sana kwa kushindwa kukujibuni maswali yetu kwa wakati, kwa kweli nimebanwa haswaa na wiki ijayo tu naanza likizo nje ya nchi, lakini Tweety mada yako ya kukuroma sijasahau na nikipata muda tu nitakujibu, anonymous nawe pia ntakujibu kwa haraka.

The great said...

pole na kazi za kila siku,Ahsante sana kwa somo hili la maji nimejufunza mengi na nitawaelimisha wengine ili wafaidike zaidi,usichoke kuendelea kutuelimisha katika afya zetu,mungu akutie nguvu.

Anonymous said...

Tafadhali tuwekee MENU NZURIII YENYE VIRUTUBISHO VYOTE YA KUPUNGUZA MWILI, MAANA NYINGI NAZIONA ZINAKUWA ZINA MAPUNGUFU FULANI FULANI

ASANTE

Paul Akwilini said...

Mimi nina mtoto mchanga. sa je? mtoto mchanga nae anahitaji maji anapofikisha mda gani? mr. merina au baba jacklina.

Shally's Med Corner said...

Mr. Merina maziwa ya mama yanatosha kwa mtoto hadi miezi minne! nasisitiza tena miezi minne! kwani maziwa ni asilimia ngapi maji? labda nusu au zaidi? basi maji ya nini tena? hakuna ulazima wa kumpa mtoto maji au chakula kingine chochote hadi afike miezi minne, tumbo la mtoto ni dogo sana na unapompa maji ambayo tayari anayapata kwenye maziwa anayokunywa basi humzuia mtoto kunyonya na kupata virutubisho muhimu katika maziwa ambavyo anavihitajia sana katika umri wake huo mdogo...

Anonymous said...

Mimi ni mdau mzuri wa kona ya afyakwani inanisaidia sana kuapata elimu mbali mbali...
naomba ushauri kuhusu matumizi ya poda kwa watoto wadogo, mana nasikia watu wengine wanasema poda si nzuri kwa afya ya mtoto...sasa nipo njia panda mana karibu nitajifungua na sielewi which is which.

Ahsante

Anonymous said...

Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* bahati nzuri
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159