Sunday, December 20, 2009

Njia za kuondoa makovu


Kuna matatizo malimbali ya ngozi yanayoweza kuwapata watu ambapo makovu ni mojawapo ya matatizo hayo.Makovu baadhi ya wakati hajawezi kuepukika hasa iwapo makovu hayo yamesababishwa na magonjwa au ajali mbalimbali. Makovu katika sehemu mbalimbali za mwili huweza kufunikwa na kufichwa kwa urahisi iwapo hayapo katika sehemu zinazoonekena. Lakini iwapo makovu yatakuwa usoni, mikononi au kifuani, huwa si rahisi kuyaficha na mara nyingi huwakera wale walio na makovu. Watu wengi wangependa kujua ni njia gani ambazo mtu anaweza kutumia ili kuondoa makovu. Ili kulijibu swali hilo ni bora kwanza tujue kovu ni nini hasa. Kovu katika mwili hutokea pale tishu aina ya fibrous inapojikusanya juu ya ngozi ili kusaidia kukarabati seli na ngozi iliyoharibika. Wakati kunapotokea jeraha, ngozi kutoa seli ziitwazo fibroblasts ambazo hutoa kitu kiitwacho collagen na kujaza sehemu yenye jeraha. Collagen ni ngumu, iko kama ufumwele unaopatikana katika protini ambayo hujaza eneo lote le kovu. Collagen ipo pia katika ngozi ya kawaida lakini katika kovu huwa nyingi na iliyojipanga katika mpangilio holela. Hii ndio sababu kovu huwa na rangi iliyokolea na huonekana kwa urahisi. Baadhi ya makovu huondoka kwa urahisi, baadhi huchukua miezi na hata miaka, huku makovu mengine yakibadilika polepole rangi na muonekano wake. Kovu huenekana kirahisi juu ya ngozi kwa sababu seli zilizotumika kuunda kovu hutofautiana na seli za mwanzo za ngozi. Kwa mfano makovu yaliyo juu ya ngozi hayawezi kuota vinyeleo kwa kuwa seli zake hazina matundu ya vinyeleo. Pia makovu hayana uwezo wa kuzuia miale ya jua. Kwa bahati mbaya ni vigumu kidogo kuweza kuondoa baadhi ya makovu moja kwa moja katika ngozi. Ingawa kuna njia kama vile vipodozi vinavyoweza kuziba makofu na njia nyinginezo za kitiba, lakina hata hivyo njia zote hizo mara nyingi huwa haziwezi kuondoa baadhi ya makovu kabisa, hasa yale makovu yaliozama katika ngozi na kuharibu kwa ngozi kwa kiasi kikubwa. Njia za tiba zinazoweza kutumiwa kuondoa makovu ni kama vile operesheni ya Laser (laser sugery), sindano za steroid, kubandua ngozi ya juu (dermabrasion) na radio therapy.
Lakini hata hivyo kuna njia mbalimbali za tiba asilia ambazo zinaaminika kuweza kusaidia kuondosha makovu. Njia hizo ni kama
1. Majani ya Aloe Vera. Majani haya yanapatikana kila sehemu hasa kwetu Tanzania na kwingineko Afrika. Majani hayo pia ni dawa nzuri ya kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi kama vile kiba au kishilingi. Kata majani hayo na utumie utomvu wake kupaka katika makovu. Baada ya muda polepole itapunguza na kuondoa makovu. Aleo Vera ni majani ambayo yanasifika hivi sasa ulimwenguni kote kwa ajili ya ngozi na yanatumiwa katika vipondozi mbalimbali. Basi zaidi ya kukuondoa makovu, yatasaidia pia kuifanya ngozi yako iwe nyororo.
2. Njia nyingine ni kutumia tango. Twanga tango na tumia mchanganyiko wake kupaka juu ya kovu. Husaidia kulainisha makovu na unapotumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.
3. Kupaka asali juu ya kovu na kuiacha usiku kucha. Njia hii inaweza kurudiwa mara kwa mara hadi pale kovu litakapotoweka.
4. Kula vyakula vyenye vitamin E, ambavyo ni ni muhimu katika kusaidia ngozi kupona na kurudia katika hali yake ya kawaida. Vitamin E iko katika mayai, nyungu za aina mbalimbali kama karanga, mayai, mafuta ya nafaka na vinginevyo. Kama huwezi jitahidi utumie vidonge vya vitamin E lakini baada ya kupata ushauri wa daktari.
5. Kupaka baking soda kidogo na maji sehemu yenye kovu na kuikanda sehemu hiyo kwa dakika moja. Mara mbili kwa siku. Kisha safisha kwa maji ya vuguvugu halafu paka mafuta ya zaituni.
6. Kutumia cream zenye vitamini E nad C na upake moja kwa moja katika kovu. Husaidia ngozi kuota tena katika kovu. Unaweza kumuona mtaalamu wa magonjwa ya ngozi naye akakushauri ni cream gani utumie ili kuondoa makovu yako. Pia jitahidi kupata lishe nzuri bila kusahau matunda na mboga mboga ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya ngozi. Kunywa maji ya kutosha kwani maji pia kulainisha ngozi yako na kufanya makovu kutoka kwa urahisi.

Inafaa kujua kuwa baadhi ya makovu kama vile yaliyosababishwa na kuungua au kuchanjwa ni vigumu kuyaondoa kwa kutumia njia hizo zilizotajwa.

14 comments:

Anonymous said...

Ni aina gani ya asali inayotumika,maana kuna asali mbichi na zingine sio mbichi.

Unknown said...

Nina kovu la kuungua mguuni na lina miaka isiyopungua 10 yaan linanikera sana. Nahitaji sana kukuondoa ila nashindwa

MESHACK YOHANA said...

NINA MAKOVU MIGGUNI KWASABBU YA KUCHEZA MPIRA NA HII INANILETEA PICHA MBAYA HATA NASHINDWA KUVAA KAPTULA YAAN INANIBOA SANA

Unknown said...

Mm nilipata ajali na nikapata kovu eneo la begani na lina zaidi ya miaka 15 je nitumie dawa gn kuondoa hilo kovu?

Unknown said...

Naomba kuhuliza mm nilipt ajali kichwan na mikfanyiwa operation kichwan Kuna uwezokano wa kuondoa kovu Hilo

Unknown said...

Makovu ya vidonda yaani malengelenge ya muda yanaweza pona pia

Unknown said...

Nimeshonwa uson na kwenye paji la uso nlichomwa visu na vibaka kidonda kina wiki tatu tokea nimeshonwa je ninaweza kuanza kutumia alovera na kuna dawa ingine ya kuondoa makovu haya ?msaada plz

Unknown said...

Mm nina makovu miguuni yalitokana na areg pia yanaweza kutoka kwa dawa izo zilizotajwa?

Anonymous said...

Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159

Anonymous said...

Nataka niondoe kovu la chanjo ya utotoni nifanye je wakuu?


Anonymous said...

Hiiii
Ulifanikiwa kupata dawa ya kovu?????

Anonymous said...

Wakuu naitaji kuondoa kovu la chanjo nifanyeje???

Anonymous said...

Nina kovu uso mzima nifanyeje?

Anonymous said...

Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
Nitaendelea kushukuru milele.
Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
. Usaidizi wa kurejesha ndoa
. Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
. Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
. Mwongozo na ulinzi wa kiroho
Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com