Sunday, March 7, 2010
Kiungulia cha ujauzito na namna ya kukiepuka
Kiungulia cha ujauzito au HeartBurn kwa kimombo ni miongoni mwa matatizo yanayowapata wanawake wengi wanapobeba mimba. Kiungulia ni hali inayopelekea mtu ajihisi kuungua au kuwaka moto sehemu ya katikati mwa kifua. Tatizo hilo huwapata wajawazito mara nyingi katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito, lakini pia wapo wakina mama wajawazito wanaopatwa na kiungulia miezi ya mwanzoni ya mimba. Ili kuelewa namna ya kuzuia kiungulia kisitokee ni bora kwanza tufahamu kiungulia kinasababishwa na nini wakati wa mimba. Kiungulia hutokea wakati kiwambo au valvu kilichopo kati ya tumbo na umio (esophagus) kinapolegea na kushinda kuzuia asidi ya tumbo isipenye na kurejea katika umio. Mimba huongeza kiungulia kwa sababu homoni ya progesterone hulegeza kiwambo hicho. Hivyo asidi inayozalishwa tumboni hasa baada ya kula hurejea katika umio na kuleta kiungulia. Kiungulia hutokea katika miezi mitatu ya mwisho ya mimba kutokana na fuko la uzazi kuwa kubwa na kubana utumbo mdogo na tumbo. Mbano huo wa tumbo hupelekea vilivyoko tumboni kusukumbwa upande wa umio au esophagus.
Kwa kawaida kutokula vyakula vyenye kusababisha asidi na gesi tumboni, hupunguza kiungulia. Vyakula hivyo ni kama vinywaji vyenye gesi ya carboni, vyakula vyenye kiasi kikubwa cha asidi kama vile jamii ya maharagwe kama maharagwe, kunde, mbaazi n.k, nyanya, vyakula vyenye viungo, matunda kama machungwa na juisi ya machungwa, chocolates, vyakula vyenye mafuta mengi, grape fruit na hata kitunguu swaumu. Lakini pia inategemea mtu na mtu inabidi ujichunguze na kuona ni vyakula gani ukila unapata kiungulia na gesi.
Zifuatazo ni njia za kujiepusha na kiungulia:
1. Kutumia baadhi ya dawa salama zinazozuia kiungulia na gesi wakati wa ujauzito. Kwa nchi zetu za Afrika Mashariki sote tunaifahamu dawa iitwayo Magnesium ambayo husaidia kuondoa tatizo hilo. Kama upo nchi nyinginezo pia natumaiani unaweza kupata dawa hiyo kwa msaada wa daktari wako. (Muhimu ni kupata ushauri wa daktari utumie dawa gani ya kuondoa heartburn au kiungulia ambayo ni salama wakati wa ujauzito).
2. Hakikisha unakula kiasi kidogo cha chakula na usile ukashiba sana. Kwa kuwa mama mjamzito huwa anasikia njaa mara kwa mara na anahitajia kula vyema ili aujenge vizuri mwili wake na watoto, basi ni bora chakula chake ukigawe katika sehemu kadhaa ndogo, na ale mara kadhaa, badala ya kula sana wakati mmoja. Suala hilo litafanya tumbo lake lisijae na kusaidia kuzuia asidi isipande juu ya tumbo na kusababisha kiungulia na gesi.
3. Jitahidi usinywe maji mengi sana baada ya chakula au wakati wa kula, kwani husaidia kuzalisha asidi tumboni kwa haraka na kuleta kiungulia.
4. Unaweza kula ubani au chewing gum baada ya kula, kwani ubani kutengeneza mate na mate hupunguza asidi.
5. Jitahidi usilale tu mara baada ya kula, subiri kama nusu saa hivi ipite ndio ulale. Unapolala usilaze kichwa moja kwa moja bila mto, bali tumia mito kuegemeza kichwa ili kuzuia asidi isirejee juu ya tumbo na kusababisha kiungulia.
Unapohisi kiungulia kunywa glasi ya maziwa au kula mtindi.
Na kama hali hiyo haijatoweka kunywa maji ya moto glasi moja yaliyowekwa kijiko kimoja cha asali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
9 comments:
Hi, Naomba msaada wako tafadhali, mimi ni mjamzito wa miezi karibu 5 na sijui ni aina gani ya mazoezi ambayo ninapaswa kufanya, nisaidie pls mana asikia nisipofanya mazoezi naweza kupata shida wakati wa kujifungua.
Pia kuna tetesi nimesikia kuwa eti ukibana mkojo kwa muda mrefu utaweza kumuunguza mtoto na kuzaliwa akiwa na mabaka meusi mwilini?
Naomba majibu pls kama unaweza unitoe hofu.
Mdau
Ndugu mdau, kwanza samahani kwa kukujibu baada ya muda mrefu kupita, hii ni kutokana na kutingwa na shughuli. Pili naomba niruhusu nilijibu swali lako la kwanza kwa undani katika makala kwenye blog. Na tatu kuhusiana na swali lako la pili, tetesi hizo si kweli. Mtoto akiwa tumboni anahifadhiwa katika mfuko wa uzazi na kukingwa asipatwe na madhara mbalimbali. Kibofu cha mkojo kiko mbali na mtoto aliko na wala mabaka anayozaliwa nayo mtoto hayasababishwi na kuunguzwa na mkojo.Ondoa wasiwasi kuhusiana na suala hilo, bali jitahidi kila unaposikia mkojo basi usiubane muda mrefu hii ni kwa faida yako mwenyewe.Hizo ni tetesi zisizo na msingi kama zile za mama mjamzito kukatazwa kula mayai.
Nashukuru sana kwa msaada wako. Pia nimefurahi sana umetoa mada ihusuyo ujauzito na mazoezi nimepata mwanga kwa kweli mana mimi ni mtu wa kushinda ofisini nimekaa so nitajitahidi kufanya mazoezi ya kutembea kila ninapopata muda maana mimi sikuwa mtu wa kufanya mazoezi kabla ya ujauzito.
God bless you
God Bless you too mdau
nimepata mwanga ndg yangu, je ni nini kinasababisha mimba kutoka? endapo huna jambo lolote la kuashiriakuitoa?
Pole na kazi. Nina ujauzito wa wiki kama 11 natapika sana mpk nahofia kula. Kivhefuchefu natembea na kopo LA kutemea mate. Nifanyeje? Asante
Ila izo unazozita "TETESI ZISIZO NA MSING" zinamaana japokuwa wazee wa zamani walikuwa wanashindwa kujenga hoja zenye mantiki kutokana na ufinyu wa elimu japokuwa makatazo yao yalikua yanamaana.UKWELI USIOPINGIKA MAYAI HUSABABISHA GESI TUMBONI
Habari ya kazi mm naomba kuuliza mama mjazito akila kidogo tumbo linajaa sana hali hiyo inasababishwa na nn?
Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159
Post a Comment