Saturday, August 7, 2010

Je, Poda zina madhara kwa watoto?


Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, Kona ya Afya imeamua kuanza tena kutoa makala kwa ari mpya, ambapo kwanza tunaanzia kwa kuwajibu maswali wadau ambayo yaliulizwa huko nyuma. Hivyo napenda kuwaeleza wale waliouliza maswali yao kuwa, wasifikiri nimeyatupa kapuni bali nitayajibu moja baada ya jingine Mungu akijaalia.
Tukirudi katika swali la mdau aliyeuliza je Poda zina madhara kwa watoto, kwanza tujue poda ni nini?
Poda ya watoto ni unga unga unaotumika ili kuzuia vipele vya nepi kwa watoto na wakati mwingine hutumika kwa ajili ya kuondosha harufu kama deodorant na kwa matumizi mengine ya vipodozi. Poda inaweza kuwa imechanganywa na 'talc' ambapo poda ya aina hiyo huita talcum powder, na wakati mwingine huchanganywa na unga wa wanga. Poda ya Talcum ni hatari iwapo itamezwa na mtoto kwa sababu inaweza kusababisha pneumonia au ugonjwa wa granuloma. Hakuna maelekezo ya moja kwa moja ya madaktari au taasisi zinazohusika kwa mfano WHO kuhusiana na madhara ya poda kwa watoto au kupiga marufuku matumizi ya poda kwa watoto. Lakini kuhusiana na aina ya poda za Talcum baadhi wanasema kwamba, talc ni mada inayoweza kusababisha kensa na magonjwa mbalimbalia kama vile cysts. Pia wanasema kwamba poda aina ya talc ni hatari kwa mtoto iwapo ataimeza au itamwingia mtoto mdomoni. Lakini pia wako wengine wanaosema kuwa hata poda ya wanga nayo ikitumiwa kwa ajili ya kupunguza vipele vya nepi huweza kuzidisha maambukizo ya 'yeast' au fungus. Vilevile kuna wengine wanaosema kwamba kwa kuwa mwili wa mtoto bado ni mchanga na dhaifu, kujiepusha kutumia katika ngozi ya mtoto vitu vinginevyo kama poda au hata mafuta huweza kusababisha mtoto apate allergy hasa iwapo vifaa kama hivyo vitakuwa vimepitwa na wakati au havikuhifadhiwa katika hali nzuri. Lakini la muhimu kabisa ambalo madakatari, wauguzi na wakunga huwahusia wazazi hasa baada ya kuzaliwa mtoto ni kujihadhari iwapo wanatumia poda wahakikishe kuwa poda haingii kwenye kitovu cha mtoto kabla hakijaanguka.
Hivyo ndugu mdau uliyeuliza swali hili, sina jibu la moja kwa moja kwamba poda ina madhara au la, ispokuwa nakuachia mwenyewe baada ya kusoma makala hii uamue utumie poda kwa ajili ya mtoto wako au usitumie.
• Lakini iwapo utataka kutumia poda basi naweza kukushauri tu ni bora unaponunua poda basi na uangalie vyema kabla ya kununua na kuhakikisha kwamba si ya talcum. Na kama utatumia ya wanga basi iwapo mtoto atapata fungus kwa wakati huo usiendelee kutumia poda hadi atakapopona. Kwani kuendelea kutumia poda kunafanya fungus zizidi.
• Pia hakikisga poda haiingia katika kitovu cha mtoto hasa wakati kibichi na kabla yakijaanguka.
• Hakikisha mtoto hamezi poda au poda haimuuingia mdomoni, puani au masikioni.
• Hakikisha unanua aina za poda zinazojulikana vyema kutoka katika mashirika yenye itibari.
• Hakikisha hata kama unanua poda yenye jina linalojulikana lakini usinunue sehemu mbazo poda humwaga chini au huhifadhiwa katika sehemu zisizofaa ambapo huweza kusababisha hali ya awali ya poda ibadilike.
• Zingatia muda wa kuisha matumizi ya poda unayoitumia, expire date.

3 comments:

Anonymous said...

Nashukuru sana kwa kunielimisha kuhusu matumizi ya poda...at least i know where to stand.

Ubarikiwe sana.

Mdau.

pam said...

jamani mi nadhani tungeacha kabisa matumizi yake...kwani mi nadhani unapoacha haina madhara makubwa kama kuendelea kutumia..tena huo unga wa talcum kuna tetesi pia ukawa ni source ya magonjwa ya pumu/athma kwa watoto wengi...tujitahidi kuelimishana itaenea tutaelewa.as iknw ni ngumu kwani wengi wetu tumekuzwa na hizo hizo poda sasa leo hii kumwambia mama yako usimpake mwanagu poda hatakuelewa.sanasana mpake mafuta yake sehemu hizo zenye mikunjo kuepuka ukavu..mfano wa mmafuta hayo ni olive oil ni mazuri na hayana harufu na ni ya asili kabisa

ODACE BALIMPONYA said...

Ahsante kwa elimu nzuri.