
Kwanza nawatakiwa wadau Waislamu wa Kona ya Afya swaumu njema na kw amanasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani nimeandika makala hii kuhusiana na umuhimu wa kufunga. natumaini mtafaidika nayo.
Kufunga kumeamriswa katika dini mbalimbali ikiwepo dini tukufu ya Uislamu, Uyahudi na Ukiristo. Mbali na dini mbalimbali kuamuru wafuasi wao wafunge kama moja ya ibada muhimu, wataalamu wengi wa masuala ya tiba wamekuwa wakiamini kuwa kufunga ni miongoni mwa tiba asilia na inaleta faida kubwa kiafya. Kufunga kuna faida tele kwa afya na kwa siha ya mwili. Uislamu unawataka wafuasi wake wawe wenye afya njema, wasafi, walio imara kiimani na kimwili na mwenye nguvu. Bwana Mtume Mtukufu Muhammad (S.A.W) ametilia nguvu hoja hiyo pale aliposema kwamba: "Fungeni mpate siha".
Hii leo pia wataalamu wa masuala ya afya wamethibitisha faida kemkem mtu anazoweza kuzipata mtu kwa kufunga, zinazouinufaisha mwili na akili. Kuna baadhi ya madaktari wanasema kuwa kufunga kunamfaidisha mtu kisaikolojia na kimwili. Mbali na swaumu kumfanya anayefunga awe na stamina ya njaa na aweze kuvumulia matatizo na awe na subra, pia husaidia kupunguza mafuta ya zaida mwilini. Faida za kufunga haziishiii hapo bali pia swaumu ni njia ya kuponya magonjwa mbalimbali yakiwemo yale yanayohusiana na mfumo wa chakula kama vile maumivu ya tumbo sugu, kuvimba utumbo mkubwa, ugonjwa wa ini, kukosa choo na matatizo mengineyo kama vile unene wa kupindulia, kuziba mishipa ya moyo (arteriosclerosis), shinikizo la damu, asthma, diphtheria na kadhalika.
Lakini kabla hajujaendelea na mada yetu hii hebu sasa tueelezee kwa undani kitaalamu jinsi kitendo cha kufunga kinavyoufaidisha mwili.
Kufunga kitaalamu huanza pale mwili unapokosa chakula kwa masaa 12 hadi 24. Kikemia kufunga hakuanzi hadi pale sukari aina ya carbohydrate iliyohifadhiwa mwilini inapoanza kutumiwa kama chanzo cha kuzalisha nguvu. Kufunga huko huendelea madam tu mafuta na carbohydrate iliyohifadhiwa iendelee kunyofolewa na badilishwa kuwa nguvu, bila kutumiwa protini iliyohifadhiwa. Pale protini inapoanza kutumiwa na kubadilishwa kuwa nguvu (suala ambalo hupelekea misuli kupungua) kitaalamu tunasema kuwa mtu ameanza kukabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula mwilini au kwa kimbombo starving.
Faida za kufunga zinaweza kufahamika kwa kujua jinsi mwili unavyofanya kazi wakati chakula kinapokosekana.
Wakati mwili unapoishiwa na nguvu inayotokana na chakula, huanza kutegemea hazina yake ya chakula kilichohifadhi na kitendo hicho huitwa Autolysis. Autolysis ni kuvunja vunja mafuta yaliyohifadhiwa mwilini ili kutengeneza nguvu, kitendo ambacho hufanywa na ini. Hali hiyo hupunguza mafuta ya ziada mwilini ambayo ndio sababu kuu ya magonjwa mengi kama vile shinikizo la damu, mshituko wa moyo na kadhalika.
Kufunga pia husaidi kuondoa sumu mwilini. Suala hilo hurahisishwa na kufunga kwani chakula kisipoingia mwilini, mwili hubadilisha mafuta yaliyohifadhiwa kuwa nishati na kupitia kitendo hicho kemikali nyinginezo na sumu zenye madhara kwa mwili pia hutoka katika utumbo, ini, figo, mapafu na ngozi. Hizi ni sumu ambazo hutokana na vyakula tunavyokula na mazingira yetu, na huingia mwilini na kuhifadhiwa pamoja na mafuta.
Faida nyingine ya swaumu kitiba ni kuupumzisha mfumo wa chakula. Wakati mtu anapokuwa hali, nguvu inayotumiwa na mfumo wa chakula ambao huwa umepumzika huelekezwa kwenye metabolism na mfumo wa kulinda mwili. Kitendo hicho husaidia mfumo wa kulinda mwili uweze kufanya kazi zake vyema zaidi na kupambana na mgonjwa au vile visivyotakiwa mwilini. Pengine hii ndio babu wanyama wanapopata jeraha huacha kula, na wanadamu hupoteza hamu ya kula wanapopatwa na magonjwa kama vile mafua. Kwa sababu mwili huielekeza nguvu yake yote kwenye mfumo wa ulinzi wa mwili ili kupambana na vijidudu. Faida hiyo mtu huipata pia anapofunga.
Wakati wa kufunga vilevile joto la mwili hupungua kwa kiasi kikubwa. Hii hutokana na kupungua kasi ya metabolism na kusimama kazi nyingi zinazofanywa na mwili. Kwa kupungua kiwango cha sukari au glukosi katika damu, mwili hutumia glukosi inayohifadhiwa kwenye ini. BMR (basal metabolis rate) hupungua ili kuhifadhi nishati mwilini. Pia homoni mbalimbali huzalishwa wakati mtu anapokuwa amefunga zikiwemo homoni za kukua na za kuzuia seli zisizeeke. Hivyo njia mojawapo ya kuzuia uzee na kuwa na maisha marefu ni kufunga.
Kwa kuzingatia maelezo hayo yote tunaweza kusema kuwa, swaumu ina faida kubwa kiafya kwa mwanadamu.
5 comments:
somo zuri sana. maana sisi tunaoishi mijini, tunakula vitu vingi vyenye sumu, kama mafuta ya kula, chips na vyakula vingi vya madukani.
Mashallah Allah akuzidishie, asante sana, umetufungua sana
mamy jamani dawa ya kukoroma.
Sikuweza kushika mimba kwa miaka 10 kwenye ndoa yangu, nilikuwa kwenye ukingo wa kupoteza ndoa yangu kwa sababu mume wangu alihitaji mtoto wa kumzaa, mwenzangu wa kazi alinielekeza kwa Dr Dawn, Alikubali kunifanyia tambiko la ujauzito, nilifuata maagizo aliyonipa, na pia mshangao wangu, nilipata ujauzito ndani ya wiki 6, mimi na mume wangu tukafanya mtihani na matokeo yakaonyesha mapacha, Lakini sasa nina wavulana wangu 2 warembo, zote namshukuru Mungu Mwenyezi kwa kumtumia Dk Dawn kusaidia ndoa yangu,
Ninampendekeza Dr Dawn, kwa yeyote aliye na masuala ya uhusiano/ndoa au utasa, Dr Dawn hakika atakusaidia, wasiliana naye kwa Whatsapp: +2349046229159
Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.
Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.
Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
Nitaendelea kushukuru milele.
Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
. Usaidizi wa kurejesha ndoa
. Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
. Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
. Mwongozo na ulinzi wa kiroho
Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com
Post a Comment