Thursday, August 5, 2010

Zijue siku zako za kushika Mimba



Nimeamua kuandika makala hii ili kujibu swali la moja wa mdau wa blogi hii ambaye ameuliza kwamba, anahitaji kushika mimba na je, kwa mfano mwezi huu alianza period yake tarehe 17 Juni, ni zipi siku zake za kushika mimba? Ndugu mdau kwanza kabisa nachukua nafasi hii kukuomba samahani kwa kuchelewa kujibu swali lako. Pengine ninapoandika makala hii utakuwa tayari umeshashika mimba, basi kama ni hivyo hakuna tabu bali natumaini swali lako litakuwa limewasaidia wengine ambao pengine wana tatizo kama halo. Pia umeualiza je, ukitaka mtoto wa kike ufanyeje?
Nachukua nafasi hii kwanza kujibu swali lako la kwanza kabla sijaenda kwenye swali lako la pili. Kwani kuelewa vyema swali la kwanza kutasaidia kuelewa swali la pili pia.
Inafaa tufahamu kuwa ili kuweza kujua ni siku zipi za mwezi mwanamke anaweza kushika mimba (to conceive) inabidi tujua kwanza kipindi ambacho mwili wa mwanamke uko tayari kushika mimba au Ovulation Period. Ovulation ni wakati ambao yai lililokua hutoka katika mirija ya ovari katika kizazi cha mwanamke na katika wakati huu uwezo wako wa kushika mimba ni mkubwa. Kwa kawaida mwanadamu huwa na mayai kadhaa katika ovari zake kwa wakati maalum wa mwenzi, ambapo yai kubwa kuliko yote huondoka na kueleka katika tumbo la uzazi kupitia mirija ya ovari. Ovulation haifuati mpangilio maalum kati ya ovari katika kila mwezi na haijulikani ni ovari gani itatoa yai kila mwezi. Wakati yai linapotoka huwa na uwezo wa kurutubishwa au kukutana na mbegu ya kiume na kuanza kutengeneza mtoto kwa muda wa masaa 12 hadi 24, kabla halijapoteza uwezo wake. Iwapo yai litafanikiwa kurutubishwa na mbegu ya kiume kwa wakati maalum na kujikita katika fuko la uzazi basi matokeo yake ni mimba. Na iwapo halitorutubisha yai hilo pamoja na kuta za kizazi huharibika na kutoka nje ya mwili kama damu ya hedhi.
Nimetangulia kueleza haya kama utangulizi kabla ya kuzieleza siku za kushika mimba kwani kuelewa suala hilo kutatusaida kujua umuhimu wa kujua idadi ya siku zetu za mzunguko wa mwezi (Menstrual Cycle) na umuhimu wake katika kushika mimba na hata katika magonjwa ya wanawake. Ili kuelewa vyema siku hizo inatubidi tujue kitu kinachoitwa Kalenda ya Ovulation au kalenda ya kubeba mimba na pia tujua mzunguko wetu wa hedhi una siku ngapi. Mzunguko wa mwezi ni siku ya kwanza unayopata damu yako ya hedhi hadi siku kabla ya kupata tena hedhi nyingine.



Wataalamu wanatuambia kuwa ili kujua mzunguko huo vyema inatubidi tuchunguze hedhi yetu kwa miezi isiyopungua 6. Lakini kama una haraka na huwezi kuchunguza kwa miezi 6 chunguza kwa miezi mitatu. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia kalenda ya kawaida na kwa kuziwekea mduara kwa kalamu siku zako za mwezi, yaani siku ya kwanza ya kupata damu ya hedhi hadi siku ya mwisho kabla ya hedhi inayofuata. Mzunguko wako wa mwezi ni siku ya kwanza ya hedhi hadi siku ya kabla ya kuanza hedhi nyingine. Kwa mfano iwapo nimepata siku zangu tarehe Pili Julai na nimepata tena siku zangu tarehe 29 Julai, mzunguko wangu ni wa siku 28. Kwa kawaida mzunguko wa siku 28 ndio mzunguko wa kawaida kwa wanawake wengi. Lakini kuna baadhi ya wanawake huwa na mzunguko wa chini ya siku 28 na wengine huwa na mzunguko wa hadi siku 35.
Ni vipi utazijua siku zako za Ovulation
Wakati wa Ovulation katika mzunguko wa mwezi huainishwa na luteal phase, katika mzunguko wako. Unaweza kujua muda wa Ovulation katika mzunguko wako wa mwezi kwa kutoa idadi ya siku za luteal phase. Katika kuhesabu huko utapata mzunguko mfupi na mrefu. Chukua mzunguko mfupi wa mwezi na hesabu idadi ya siku katika mzunguko huo. Toa 18 katika mzunguko huo na utapata idadi fulani. Halafu anza kuhesabu siku yako ya kwanza ya mzunguko wa hedhi katika mwezi unaofuata kwenda mbele hadi kufikia namba ulioyopata, hivyo utaweza kupata siku ambayo una uwezekano mkubwa wa kubebea mimba.
Kwa mfano mzunguko wako mfupi ni siku 29, unatoa 18 katika 29 na unapata 11. Iwapo siku yako ya kuanza hedhi mwezi ujao ni Oktoba 3, ongeza siku 11 kuanzia siku hiyo. Hivyo siku ambayo una uwezekano mkubwa wa kubeba mimba itakuwa Oct. 14.
Halafu chungua idadi ya siku za mzunguko wako mrefu wa hedhi. Toa siku 11 kutoka katika idadi ya siku za mzunguko huo na utapata namba fulani. Halafu tena anza kuhesabu katika mzunguko wako ujao wa hedhi kwenda mbele hadi kufikia siku ambayo una uwezekano wa kupata mimba.
Kwa mfano iwapo mzunguko wako mrefu ni siku 31, toa 11 katika mzunguko huo na utapata 20. Iwapo hedhi yako ijayo inaanza tarehe 3 Oktoba, ongeza siku 20 kuanzia siku hiyo na tarehe 23 Oktoba itakuwa siku yako ambayo una uwezekano mkubwa wa kubeba mimba.
Kwa utaratibu huo utakuwa umepata kipindi cha kati ya Oktoba 14 hadi 23 ambacho ni siku ambazo una uwezekano mkubwa wa kubeba mimba au Ovulation window kwa kimombo.
Ovation huweza kubadilika kidogo katika mzunguko wako wa hedhi kwa sababu Ovulation huweza kucheleweshwa na sababu mbalimbali kama vile wasiwasi au fikra nyingi, ugonjwa, lishe au kufanya mazoezi.


Vipi kipindi cha Ovulation kinaainisha ziku za kubeba mimba?
Kipindi cha kubeba mimba huanza siku 4 hadi 5 kabla ya Ovulation, na humalizika masaa 24 hadi 48 baada ya hapo hii ni kwa sababu muda wa ovulation huweza kuchelewa au kuwahi kutokana na sababu mbalimbali. Pia kwa sababu mbegu ya kiume huwa na uhai kwa siku 4 hadi 5 na yai huweza kuishi kwa masaa 24 hadi 48 baada ya kuingia katika tumbo la uzazi. Hivyo kwa kujua siku hizo humsaidia mwanamke kufahamu kipindi chake cha Ovulation kimewadia na hivyo kuweza kukukutana na mumewe au mwenza wake wakati huo ili aweze kubeba mimba. Pia kujua kipindi hiki na masuala mengineyo kama hali ya joto la mwili ilivyo wakati wa Ovulation huweza kutumika kama njia ya kuzuia mimba. Yaani kutojamiiana katika kipindi hiki huweza kumzuia mtu asipate mimba.
Kwa kuwa kipindi cha Ovulation hakina tarehe maalum na ni siku kadhaa, katika makala ijayo nitaendelea kuzungumzia baadhi ya alama za mwili zinazosaidia kutambua ni wakati gani Ovulation imewadia.
Daima tuzilinde afya zetu!

36 comments:

Disminder orig baby said...

Sasa umerudi mtamboni, asante sana, hili darasa litatusadia wengi sana, Mungu akuzidishie. Amen

Shally's Med Corner said...

Tupo pamoja Tweety, na hilo ndilo jukumu letu.

Anonymous said...

tunshukuru kwa mada nzuri ya kushika mimba tunaomba uiendeleze tuone mwisho inakuaje.

Anonymous said...

Ahsante sna jamani, mada imenigusa manake niko ktk mchakato wa kutafuta mimba, i lyk watoto. plz mada isonge mbele.

Gg

Anonymous said...

MMMH BORA MAANA ME NDIO SIKU ZANGU ZINABADILIKABADILIKA SANA,BORA UTUPE MADA TAJUA LA KUFANYA BAADA YA KUSOMA SAN KOZ NA MIE NIPO KWENYE MCHAKAKTO WA KUTANGAZA NIA YA KUWA MENEJA MTARAJIWA

LOVE YOU DEAR

Anonymous said...

dah! cjui nikushukuruje ndugu yangu maana nilikuwa na hamu sana yakujua siku zangu, naomba uzidi kutufundisha

Anonymous said...

dah! cjui nikushukuruje ndugu yangu maana nilikuwa na hamu sana yakujua siku zangu, naomba uzidi kutufundisha

Eggy said...

kwanza pole sana majukumu ya yako ya siku nzima. ningependa kujua kitu kimoja kwa mwaka jana na mwaka huu yaani 2011 na 2012 kwa baadhi ya miezi huwa na vuka hedhi yangu ya mwezi pengine hata miezi miwili na ikija maumivu ya tumbo na kiuno huanza hivyo hunipa wasi wasi sana je nifanyaje? kutokana na mzunguko wangu wa hedhi asante sana na ubarikiwe.

Anonymous said...

mambo dada mimi nimeanza damu zangu tarehe 19 je ni wakati upi muafaka wa kushika mimba ?

Anonymous said...

pole kwa majukumu. mie mzunguko wangu unabadilika kila wakati. naomba unisaidie kama nataka kupata mimba nilinza hedhi tarehe 01 jan.2013 zipi ni siku za kushika mimba hasa mtoto wa kike? ahsante

Anonymous said...

it's a good lesson, i'm learn a thing!! Keep it up, thanx much!!!!!!!!!!!

Unknown said...

kmamzunguko wako ni siku 27 na tarehe 12february ukaingia period je siku ya kushuka mimba ni io mezi huo

Unknown said...

thanxx

Unknown said...

mi nataka kujua kam mzunguko ni siku 27 na tarehe 12 february ukaingia period je siku y kushika mimba ni ipi mwezi huo

Anonymous said...

asante aunt,hili darasa ni zuri.ubarikiwe sana

Anonymous said...


Habari yako mpendwa,nimejitahidi toka mwaka huu umeanza nishike ujauzito lkn sijafanikiwa mzunguko wangu uko hivi naingia kwenye period tarehe 20-23 jan,21-24 feb,20-23 march,22-25 april,18-21 may huo ndo mzunguko wangu toka mwaka huu umeanza je ni siku zipi sahihi kwangu ambazo naweza kushika ujauzito?

Naomba unisaidie kwa hilo

Unknown said...

mbn m2 anaweza kushika mimba siku ya saba

Anonymous said...

Mfan me naingia tareh 21 nkitoa na kujumlish mbna zinazid

agape said...

Asante kwa elimu yako nzuri uliyotupa bt mimi nina tatizo mara nyingi mzunguko wangu ni wa siku 30 but cha kushangaza sikuhizi mara nyingine mzunguko wangu unasogea mpaka siku 42 au 43 then unarudi tena kwenye 30. Sasa je tatizo linaweza likawa ni lipi na nitahesabuje tarehe za mimba?

Unknown said...

je mwanamke anaweza kupata mimbwa na akapata siku zake mfano imetokea umelala na mwanamke leo na wakati anatatakiwa kuingia kesho kwenye piriod na piriod akaipata ila ikawa na mabadiliko je kuna uwezekano akawa amepata mimba?

Anonymous said...

Mimi bado kuelewa kidogo inamaana siku ya mimba ni mika tu

Anonymous said...

I lyk hii mada coz nimejifunza mengi xan

Unknown said...

habar mm naona hedhi tarehe 8 je siku hatar ni zpi

Anonymous said...

Naomba kujua aneingia mzunguko siku 35 ni ovulation huwa sawa na anae ingia mzunguko siku 28

Unknown said...

Kuumwa chin ya kitovu siku ya kumi baada ya hedh in tatizo?

Lululinda said...

Je anaennda hedhi siku 30 ovulation yake itakuwa lini

Anonymous said...

Kwa mfano mwezi wa10 na 11 nimeingia period tarehe 10 halafu mwezi wa 12 nimeingia tarehe 26 je siku ya hatari ni ipi

Anonymous said...

Mm nmeingia piriod mwezi wa 10 na wa 11 tarehe 10 halafu mwezi huu wa 12 nimeingia tarehe 26 je siku ya hatari kwangu ni ipi?

Unknown said...

Samahani nikikuwanaomba kuliza. Je? Mwanamke anaweza kushika mimba cku mbiki kabla ya hedhi

Unknown said...

Samahani nikikuwanaomba kuliza. Je? Mwanamke anaweza kushika mimba cku mbiki kabla ya hedhi

Unknown said...

asante sana kwa mafundisho mazuri

Unknown said...

Jaman mtu akifanya mapenz tarehe 19 alafu cku yake ya menstration ni tarehe 27 je atapata mimba?

Unknown said...

Topic nzuri Sana. Asante kwa Elimu

Unknown said...

kwa hiyo mwanamke kwa mfano leo kamaliza kubread ukijamiana nae siku ya pili itakuwaje?

Anonymous said...

Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159

Anonymous said...

Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* bahati nzuri
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159