Tuesday, November 6, 2007

Jeni Inayohusisha Maziwa ya Mama na IQ


Kwa mujibu wa wachunguzi wa mjini London kuna jen moja (single gene) inayoathiri uwezo wa kiakili (IQ) katika watoto walionyonya maziwa ya mama. Watoto wenye jeni aina mojawapo ya FADS2 wanapata namba kubwa zaidi ya IQ katika vipimo vya IQ, iwapo walinyonya maziwa ya mama zao. Katika uchunguzi zaidi uliofanywa na Nationa Academic of Sience imegundulika kuwa, maziwa ya mama hayana athari yoyote katika uwezo wa Kiakili wa IQ kwa watoto ambao wana aina nyingine za jeni hiyo ya FADS2. Geni hiyo inaonekana kuwa husaidia katika kuvunja vunja chembe ndongo za mafuta zijulikanazo kama Fatty Acids katika vyakula, ambazo zimekuwa zikihusishwa na ukuaji wa ubongo. Imeonekana kuwa kuna asilimia 90 ya watu wenye aina hiyo ya jeni ambayo ina uhusiano na kupata namba kubwa katika vipimo vya IQ. Wachunguzi kutoka Kitengo cha Magonjwa ya Akili cha King College mjini London wametoa takwimu hizo katika chunguzi mbili zilizofanywa huko nyuma za unyonyeshaji maziwa ya mama kwa watoto wa Uingereza na New Zealand, zilizowashirikisha zaidi ya watoto 3,000. Profesa Terrie Moffitt mwandishi msaidizi wa makala hiyo anasema kuwa, kupakana taarifa hizi kumetoa taswira mpya katika mijadala kwa kuonyesha kuwa utaratibu wa kifiziologia ambao unaweza kutegemeae katika kuonyesha tofauti kati ya watoto wanaonyonya maziwa ya mama na watoto wanaonyonya maziwa ya chupa.

1 comment:

Unknown said...

Haya ni maajabu ya maumbile.