Tuesday, November 13, 2007

Lishe Nzuri Hupunguza Hatari ya Magonjwa ya Usahaulifu Uzeeni



Wataalamu wameonyesha ushahidi zaidi kwamba chakula chenye mafuta ya samaki na mboga mboga kinaweza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya usahaulifu baadaye katika maisha. Uchunguzi uliotolewa na jarida la Marekani unaonyesha kwamba, 'vyakula vya Mediterania' au utumiaji wa muda mrefu wa vyakula vyenye beta-carotene kunaweza kuzuia magonjwa hayo. Aina zote hizo za vyakula vina antioxidanti ambazo ni chembe chembe zinazozuia vitu au vyakula kuoza vinapoungana na oksijeni. Antioxidanti huuepusha ubongo kuharibika. Taasisi ya Alzheimer imesema kuwa watu wengi wanaweza kupunguza hatari ya magonjwa hayo kwa kula vyakula bora. Uchunguzi wa kwanza uliofanywa na jarida la Neurology umechunguza vyakula vya watu 8,000 wasio na magonjwa wanawake na wanaume walio na umri wa zaidi ya miaka 65. Uchunguzi huo umeonyesha kwamba, wale wanaokula vyakula vyenye mafuta yenye omega-3, ambayo hupatikana katika baadhi ya mafuta na samaki, watu hao wameonekana kuwa hawaweza kupata magonjwa hayo katika kipindi cha miaka minne inayofuata. Watu wanaokula samaki kwa akali mara moja kwa wiki wana punguza uwezekano huo kwa asilimi 40 huku wale wanaotumia mbogamboga mara moja kwa siku hupunguza uwezekano huo kwa asilimia 35.
Beta-carotene ni kemikali ambayo huipa rangi karoti ambayo ni aina ya ant-oxidanti.

No comments: