Thursday, November 15, 2007

Sigara Inavyoathiri Uzazi wa Wanaume





Wataalamu wanasema kuwa kuvuta sigara wakati wa mimba kunapunguza uwezo wa kuzaa kwa watoto wa kiume kwa kuathiri jeni muhimu za umbo la kiume ambapo gameti za kiume hutengenezwa au mapumbu. Tayari imeshajulikana kuwa kuvuta sigara kunaathiri uzazi wa watoto wa kiume hapo baadaye, lakini bado haijajulikana ni vipi suala hilo hutokea. Wataalamu wa chuo kikuu cha Aberdeen wamegundua kuhusiana na kupungua kwa kiwango kikubwa cha jeni iitwayo DHH ambayo ina nafasi muhimu katika ukuaji wa maumbo hayo ya kiume, katika watoto wa kiume wanaozaliwa na mama wanaovuta sigara wakati wa ujauzito. Jarida la Kliniki ya Endocrinoloy na Metabolism limeripoti kuwa pumbu ndogo zinahusiana na utengenezwaji wa manii kwa kiasi kidogo suala lenye umuhimu mkubwa katika uzazi wa mwanamume. Uchunguzi umeonyesha kuwa, watoto waliotumboni ambao mama zao huvuta sigara 10 au zaidi kwa siku , kiwango chao cha jeni ya DHH hupungua, zaidi ya watoto ambao mama zao hawavuti sigara.

No comments: