Wednesday, November 7, 2007

Operesheni ya Lakshmi Yafanikiwa!Mtoto wa Kihindi Lakshmi Tatam aliyekuwa akifanyiwa operesheni ya kupunguza viungo vilivyozidi mwilini, anaendelea vizuri. Mtoto huyo alizaliwa na miguu minne na mikono minne. Timu ya madaktari wa mji wa Bangalore imetumia masaa 27 katika operesheni hiyo ambapo walitenganisha uti wa mgongo wa Lakshmi na figo za mtoto huyo na pacha wake ambaye waligandana lakini hakukua. Madaktari hao wameelezea matumaini yao kuwa kwa kufanyiwa operesheni hiyo, Lakshmi ataweza kuishi mpaka wakati wa kubalehe.

No comments: