Tuesday, November 20, 2007

Maambukizo ya Ukimwi Yapungua, tuzidi Kufanya Juhudi!



Takwimu mpya zilizotolewa leo na Umoja wa Mataifa zimeonyesha kuwa idadi ya watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa hatari wa Ukimwi pamoja na idadi ya maambukizo mapya ya ugonjwa huo imepungua. Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Mpango wa Kupambana na Ukimwi Duniani (UNAIDS) kwa pamoja yamesema mjini Geneva Uswisi kwamba inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 33 bado wanaishi na virusi vya Ukimwi duniani katika mwaka huu wa 2007, ikiwa ni asilimia 16 pungufu kutoka milioni 39.5 iliyokadiriwa mwaka 2006. Katika mwaka huu wa 2007 karibu watu milioni 2.6 wameambukizwa upya virusi vya HIV, AIDS huku wengine milioni 2.5 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Shirika la UNAIDS linaamini kuwa kupungua kwa maambukizo ya ugonjwa huo hatari wa UKIMWI katika miaka miwili liyopita kumetokana na kufanikiwa mipango ya kupambana na ugonjwa huo. Nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika zimeendelea kuwa na idadi kubwa ya waathiriwa ambapo inakadiriwa kuwa watu milioni 1.7 wameambukiwa virusi vya UKIMWI katika mwaka huu wa 2007 katika eneo hilo.

No comments: