Monday, November 5, 2007

Karibu Kona Ya AfyaAssalam Aleykum wana blog wa Kiswahili,

Napenda kuwakaribisheni rasmi katika blog yangu ya Kiswahili ya Kona ya Afya Nikiwa kama Mtanzania, nimekuwa nimekuwa siridhishwi na hali ya maisha ya Watanzania katika masuala mbalimbali kama vile uchumi, elimu, siasa, afya na mengineyo. Katika miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishudia mmiminiko wa blog za aina mbalimbali za lugha ya Kiswahili. Kwa hakika suala hilo limekuwa likifurahisha na kuridhidhisha wengi nikiwemo mimi binafsi. Nachukua fursa hii nami pia kujiunga na wanablog wa Kiswahili duniani kwa kuanzisha Kona ya Afya. Natumai mtajumuika nami katika kutoa maoni yenu kusoma na hata kunitumia posts na makala mbalimbali ili kufanikisha blog hii. Mnakaribishwa wote!

No comments: