Tuesday, November 6, 2007

Mtoto wa Miguu Minne na Mikono Minne!


Mtoto wa India aliyezaliwa na mikono minne na miguu minne afanyiwa operesheni. Mtoto huyo mwenye miaka miwili ajulikanaye kama Lakshimi Tatma viungo vyake hivyo vimeungana toka kiunoni katika kile wataalamu wanachokitaja kuwa ni athari za pacha ambao hakuwa na kichwa na hakuendelea kukua. Timu ya upasuaji katika mji wa kusini mwa Bangalore wamesaidia katika kutenganisha viungo vya mtoto Lakshimi. Imeripotiwa kuwa mpaka sasa operesheni hiyo inaendelea vizuri. Operesheni hiyo inatarajiwa kuchukua masaa 40 mpaka kumalizika. Kwa kawaida mapacha wa kuungana hawatokei sana ambapo kunatokea kesi moja katika watoto laki mbili wanaozaliwa. Historia ya kuhifadhi data inaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka 500 iliyopita kumerikodiwa kesi 600 za mapacha wa kugandana ambapo zaidi ya asilimia 70 ya mapacha ho walikuwa watoto wa kike.

No comments: