Monday, March 9, 2009

Bibi Sara Obama kusaidia katika kampeni za kupambana na mbung'o


Umoja wa Afrika umetangaza leo kwamba Sara Obama, bibi yake Rais Barack Obama wa Marekani atatumia umaarufu wake kusaidia katika kampeni za kupambana na mbun'go, ambao wanasababisha ugonjwa wa Malalo. Timu ya AU iliyotembelea kijiji anochoishi bibi huyo cha Kogelo huko magharibi mwa Kenya imesema kuwa, Bi. Sara Obama mwenye umri wa miaka 78, amepatiwa dawa za kupambana na mbun'go pamoja na vifaa vya kutosha vitakavyotumika kuwatibu wanyama 3,000 ambao huweza kupata ugonjwa huo sawa na binadamu. Timu huyo imesema, Mama Sarah amefurahia wadhifa huo na kuahidi kwamba atakuwa balozi mzuri katika kampeni za kuwang'oa mbung'o kwenye eneo lake.
Inafaa kuashiria hapa kuwa nchi 37 za Kiafrika zinakabiliwa na mbu aina ya mbung'o ambao wanasababisha ugonjwa wa Malalo. Jitihada zinazofanywa na Umoja wa Afrika dhidi ya ugonjwa huo, tayari zimeshazaa matunda katika nchi za Botswana na Namibia.

No comments: