Saturday, March 7, 2009

Obama kuondoa marufuku ya uchunguzi wa seli mama


Rais Baraka Obama wa Marekani anatarajiwa kuondoa marufuku katika fedha za kusaidia katika utafiti kuhusiana na seli mama au stem cell. Rais aliyepita wa Marekani, George Bush alizuia kutumiwa fedha za serikali kufadhili utafiti wa seli mama za ambriyo baada ya tarehe 9 Agosti 2001.
Wanasayansi wanasema kuwa, utafiti juu ya seli mama utapelekea ugunduzi muhimu katika tiba, lakini makundi mengi ya kidini yanapinga uchunguzi huo. Seli mama ni seli ambazo zina uweza wa kugeuka na kuwa aina yoyote ya seli za mwili wa mwanadamu, kama vile mifupa, mishipa na hata seli za fahamu.
Lakini kutumiwa seli mama zinazotokana na embriyo ya mwanadamu katika utafiti huo ni suala lililozua mjadala mkubwa na baadhi ya watu wanasema kuwa, utafiti huo ni kinyume cha maadili. Tayari baadhi ya wanasayansi katika uwanja huo wameonyesha kufurahiashwa na hatua hiyo ya Obama wakisema kuwa, uchunguzi huo utaendelea tena baada ya kusimamishwa kwa miaka 8. Hatua hiyo ya Obama ni katika kutekeleza ahadi zake alizozitoa kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Baadhi ya nchi kama vile Iran zinafanya utafiti wa seli mama na tayari zimepiga hatua zaidi ikilinganishwa na Marekani kuhusiana na suala hilo,

No comments: