Monday, March 2, 2009
Kufanya kazi muda mrefu huleta usahaulifu!
Kufanya kazi kwa muda mrefu kunaongeza hatari ya kupungua kwa akili na kukumbuka mambo, suala ambalo linanapelekea kwa kiasi kikubwa mtu kupatwa na magonjwa wa usahaulifu hasa uzeeni.(dementia).
Huko nyuma uchunguzi ulionyesha kwamba kuishi maisha yasiyo mazuri, kuongezeka kwa ukosefu wa usingizi, mifadhaiko ya kimawanzo na msongo wa mambo na kutokuwa na utulivu, mambo ambayo yako katika mfululizo mzima wa kufanya kazi kwa muda mrefu, kuna uhusino na matatizo ya mishipa ya damu.
Uchunguzi uliochapishwa pia katika Jarida elimu ya Magonjwa ya mlipuko la Marekani (Epidemiology Journal of America) umeonyesha kwamba, kufanya kazi za ziada au overtime, kuna athari mbaya katika ubongo.
Kwa hivyo wale wanaofanya kazi sana wako katika hatari ya kusahau mambo lakini kwa kipindi kufupi pamoja na kushindwa kukumbuka baadhi ya maneno.
Kushindwa kufanya kazi vizuri ubongo kumeonekana kutokea zaidi kati wale wanaofanya kazi zaidi ya masaa 55 kwa wiki, suala ambalo halionekani kwa wale wanaofanya kazi kwa viwango vya kawaida.
Wanasayansi wanaamini kuwa, kufanya kazi kwa kiwango cha kawaida pamoja na kula chakula bora na kilicho kamili, maingiliano ya kijamii ya kawaida pamoja na kufanya mazoezi ya mwili na akili, kunaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya kusahau hasa uzeeni au dementia.
Haya kazi kwenu wadau, kwani hakuna anayetaka kuwasahau wajukuu zake pindi atakapozeeka. Shime tuzitunze afya zetu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment