Friday, April 16, 2010

Aspirin hutibu migreni


Wakati mauamivu makali ya kichwa au migraie yamekuwa yakitibiwa kwa dawa kali za maumivu, uchunguzi mpya umegundua kuwa dozi moja tu ya aspirini inaweza kuwaopunguzia maumivu walio na ugonjwa huo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Cochrane Library, kunywa dozi moja ya aspirini ya kati ya miligramu 900 hadi 1000 kunaweza kupunguza mauvimu makali ya migraine kwa masaa mawili. Hata hivyo utafiti huo umesema dawa hizo zinaweza kuwafaa baadhi ya watu na zisiwafae wengine na kwamba hiyo ni kutokana na tofauti ya genetiki. Kunywa dozi kubwa ya asprini kumeripotiwa kuwa na athari ya kupunguza kichefuchefu, kutapika na hata hali ya kutoweza kuvumilia mwanga na sauti (photophobia na phonophobia) hali ambazo hujitokeza kwa wale wanaopatwa na migraine.
Lakini wataalamu wamewashauri wale wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa ya migraine wajiepushe kutumia vidonge hivyo kwa muda mrefu kwani aspirini zinaweza kuleta athari mbaya kama vile matatizo ya tumbo.

3 comments:

BabyAmore said...

Thank you. kichwa wengine ndiyo matatizo yetu.

Paul Akwilini said...

Pia ungetuambia kuwa visitumike kwa muda gani? kwa mfano wanasema kwamba panadol usiitumie zaidi ya vidonge 8 kwa siku.

Shally's Med Corner said...

Bwana Paul unaposema vidonge 8 inabidi pia usema vidonge hivyo ni vya mg ngapi?.. kwa kawaida kwa wanaumbwa migrane wanashauriwa kutumia mg 900 za Asprin pale maumivu yanapoanza na kiasi hicho hutosha. Tunaposema kutumia kwa muda mrefu ina maana zaidi ya siku kadhaa au kufanya matumizi ya dawa hizo mazoea na kutumia kila siku. madhara ya dawa mara nyingi hutegemea kiasi cha dose ya dawa iliyotumika au muda wa kutumia dawa hizo.