Friday, April 16, 2010

Vifo vya kinamama vimepungua duniani

Takwimu za mwisho zinaonyesha kwamba idadi ya vifo vya kimamama vimepungua duniani kutoka nusu milioni mwaka 1980 hadi chini ya vifo 350,000 mwaka 2008. Vifo vya kinamama vinavyotokana na ujauzito au Maternal ni vifo vya kina mama vinavyotokea wakati wa ujauzito au katika siku 42 mwishoni mwa ujauzito. Vifo hivi hutokana na sababu yoyote unayohusiana na ujauzito au masuala mengine yanayoambatana na hali hiyo.


Idadi hiyo ya vifo imekuwa ikitumika kutambua na kuonyesha kiwango cha hali ya huduma za afya katika maeneo mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa uchunguzi ulioshapishwa na jarida la The Lacent, idadi ya kinamama wanaofariki dunia kutokana na matatizo ya ujauzito imepungua kwa zaidi ya asilimia 35, katika kipindi cha miaka 30 iliyopita. Hii ni katika hali ambayo nchi kama vile China, Misri, Ecuador na Bolivia zimefanikiwa kufikia malengo ya kimataifa ya kupunguza idadi ya wanawake wanaofariki dunia kutokana na matatizo ya ujazito, huku nchi za Marekani na Norway zikiripotiwa kushuhudia ongezeko la vifo hivyo. Wengi wanasema kwamba, sababu kuu iliyopelekea ongezeko la vifo hivyo katika nchi hizo mbili ambazo ni tajiri na zenye huduma bora ya tiba ni kuongezeka magonjwa miongoni mwa kinamama wajawazito pamoja na kinamama kubeba mimba katika umri mkubwa.

Vilevile imeripotiwa kwamba kwenye nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika katika kila wanawake watano wajawazito mmoja kati yao ana virusi vya HIV. Ugonjwa ambao umesababisha vifo vya watu 61,400 katika mwaka 2008. Asimilia 80 ya vifo vya kina mama wajawazito hutokea katika nchi 21 duniani ambapo India, Pakistan, Nigeria, Afghanistan, Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinachangia zaidi ya nusu ya idadi yote hiyo ya vifo vilivyoripotiwa.

2 comments:

Anonymous said...

asante kwa kazi nzuri, ila Dr. sometime utakuta wanawake wana minyama ndani ya tumbo, jje nn husababisha na nini dawa.
asante Asha

Shally's Med Corner said...

Asha, minyama hiyo kitaalamu huitwa fibroids, ambazo ni mkusanyiko wa seli zilizokuwa kutokana na mabadiliko ya homoni mwilini. kwa kweli sababu hasa inayosababisha manyama hayo kukua (kama unavyoyaita) haijulikani lakini kuna baadhi wanasema baadhi ya vyakula kwa baadhi ya watu huongeza kukua fibroids kama vile nyama, samaki na vyakula vinavyotokana na maziwa. Hivyo wenye nyama hizo ni bora waende hospitali ili wapatiwe matibabu.