Monday, October 12, 2009

Mask ya ndizi na asali kwa ajili ya ngozi zenye mafuta


Baada ya kuelezea namna ya kutengeneza mask ya Avocado ambayo ni kwa ajili ya ngozi za kawaida na zilizo kavu, hebu sasa na tuangalie namna ya kutengeneza mask ya ndizi na asali kwa ajili ya ngozi zenye mafuta na kutoka chunusi.
Vinavyohitajika
• Ndizi moja iliyoiva vyema.
• Asali kijiko kimoja cha chakula.
• Limau, ndimu au chungwa moja.

Namna ya kutengenza:
1. Menya ndizi na uiponde vizuri, kisha changanya katika kibakuli safi pamoja na asali.
2. Kamua limau, ndimu au chungwa, toa kokwa na maji yake changanya kwenye mchanganyiko wa ndizi na asali.
3. Chanyanya vizuri hadi upate mchanganyiko sawia.
4. Paka mchanganyiko huo usoni na shingoni bila kuweka machoni.
5. Wacha kwa muda wa dakika 15 na osha kwa maji ya uvuguvugu.

13 comments:

Anonymous said...

Samahani kwa maswali mpendwa, niliona sehemu wanasema kuwa kuna mask ya clay/mad ambayo ni clay inaweza kuchanganywa na maji ya limao, ndimu, asali n.k kwa ngozi za mafuta.
Sasa naomba kujua hiyo clay naweza kutumia hata udongo wa pemba ambazo wanawake wengi hupenda kula?
Na kama ni kweli hauna madhala kwa afya?
Mdau wa Musoma

Shally's Med Corner said...

Bila samahani mpendwa,
Ni kweli zipo mask mbalimbali za udongo au clay, zinazoweza kutumika kwa ajili ya uso. lakini kwa bahati mbaya mara nyingi udongo huo au clay huwa ni maalum na hutengenezwa na kuuzwa kwa ajili hiyo, si kwamba kila udongo unaweza kuutumia kama mask, bali udongo huo hutengenezwa na huongezwa madini mbalimbali zenye manufaa kwa ajili ya uso. Lakini udongo wa bahari ni miongoni mwa udongo ambao unaweza kuutumia kutengeneza mask ya clay. Kuhusiana na udongo wa pemba, ingawa sina elimu nao, lakini sikushauri kutumia kwani hatujui wanapotengeneza wanatumia vitu gani, ni bora usiutumie ili kuepusha madhara kwa ngozi yako.Vilevile wanapomaanisha mud, si tope kama tunavyodhani wala haihusiani na udongo bali ni mchanganyiko wa vitu mbalimbali ambavyo hufanya mkorogo kama tope au mud, ambayo hutumika usoni.Unaweza kuwa ndani yake udongo au bila udongo.

Mdau wa Shinyanga said...

mikorogo, mhhh. kazi ipo

Shally said...

Mdau wa Shinyanga, neno mkorogo hapa linamaanisha mchanganyiko uliokorogeka vyema, na sio maana hiyo unayoidhania wewe.

Mdau wa Shinyanga said...

Kuna tofauti gani baina ya ya hiyo Mask na ule mkorogo wa Waswahili? au na kule kujichubua? Uislamu unasema nini kuhusu hili naomba wanamblogu munisaidie.

Anonymous said...

We mdau wa shinyanga acha hizo...! Hapa hatuongelei mikorogo unayoifikiria wewe, si mikorogo ya krimu kama movate n.k + Jiki + carorite + Omo na chemical mbalimbali unazozijua wewe...!!!LOl
Hapa tunaongelea njia za asili zinazoweza kulainisha ngozi bila kukuchubua na bila kukupa madhara yoyote.
Sasa kama huwa unaweka ndimu au limao kwenye uji na unakunywa juice za limao au chungwa kuna ubaya gani ukizitumia kusafisha uso kama cleanser? HAPO UISLAMU UNAHUSUUUU??
Mask hizi hazichubui hata kidogo ni wewe tu na wasi wasi wako.

Mdau wa Musoma

Shally's Med Corner said...

Mdau wa Shinyanga Uislamu pia unashajiisha sana kutumia tiba asilia, hapa tunatunza ngozi kiasili na hakuna mkorogo au kujichubua, mask zaidi ni kwa ajili ya kuzuia ngozi isipate chunusi na isafishike vyema na sio kujichubua. naona mdau wa Musoma kakujibu vizuri. Hapa ni usafi wa uso tena bila kujichubua, suala ambalo hata uislamu unaliunga mkono pale uliposema, usilamu ni mzuri na unapenda mambo mazuri. Kama wewe ni muislamu basi unalijua hilo. usitukufurishe bure, hatujatenda dhambi yoyote kwa kuosha nyuso!

Mdau wa Shinyanga said...

wewe mdau wa musoma unajifanya hamnazo nini? kuuliza si ujinga, kwani mimi nimeshuhudia hata hiyo mikorogo ya kiswahili inafafana na hizi maski za ndizi na nyinginezo, sijakurupuka tu na kuropokwa. Halafu acha jazba,mijitu mingine bwana.. mie sijauliza kwa ubishi bali nataka kujua.

Anonymous said...

nimefurahishwa sana na jibu la Mdau wa Shinyanga kwa mdau wa Musoma. Mtu kauliza anataka kujua. Jifune kuzungumza we mdau wa Musoma

Anonymous said...

Sijaridhishwa na majibu ya Shall's Med Corner, bali naona kababaisha tu kuhusu msimamo wa Uislamu. Halafu hiyo Uislamu mzuri unapenda mambo mazuri, sijui ni aya au hadithi au ...naomba niweke wazi zaidi kwa hoja za kielimu

Anonymous said...

Wewe mdau wa shinyanga nani kakwambia mimi ninajazba? Lol utajiju mi sina jazba wala nini bishost...kama wewe ulitumia juice ya limao kusafisha uso ikakuchubua basi unamatatizo
Na kama kuuliza si ujinga basi wewe hujui kuuliza maana ulikuwa unasema hiz mask zinachubua!!! labda uliyemuona kachubuka akwambie alichanganya na kitu gani.

Jazba nikupandishie wewe??? INAHUSUUU kama unataka tumia mask asilia hutaki IPOTEZEEE uislamu na limao au tango wapi na wapi basi utaacha hata kula matunda kisa uislam.tehe tehehehehehehe
Vilivyo na mdhara hamuulizi uislam vya asili eti uislam.
Ni hayo tu.

Mdau wa Musoma

Anonymous said...

Na wewe mdau wa Shinyanga chunga mdomo wako, unawezaje kumuita binadamu mwenzio mijitu? halafu unasita kutumia mask za matunda? Huyo mungu unayemcha wewe ni yupi?
Naona wewe ndo mwenye jazba basi.

Mkorogo wa ndizi hauchubui wewe uliouona labda alieka jiki. ahahahahahaha

By Emmy

lina mbwambo said...

Ngozi yangu ni ya mafuta sikuwahi kujua cha kufanya ili kujilinda na chunusi,asante kwa somo