Wednesday, October 21, 2009

Ngozi zenye mafuta na jinsi ya kuzitunza


Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.
Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:
• Kuridhi.
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya unyevu (humidity) na hali ya hewa ya joto.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta
Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.
2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipotze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.
4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.
5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.
6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.
7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.
8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.
9. Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

5 comments:

Anonymous said...

Hizo mask za clay zinauzwa wapi?
Je mchanganyiko wa asali na juice ya limao unafaa kwa ngozi yenye mafuta?

Shally's Med Corner said...

Mask za clay zinauzwa katika ya vifaa vya urembo. Inategemea uko mji gani, kwa DSM sijachunguza kama maduka ya vifaa vya urembo pia mask wanaleta au la. lakini kuna kitu kingine kinaitwa scrub, pia ni nzuri kama utakosa mask za clay. Na scrub ziko katika maduka mengi DSM.
Kuhusu asali na limau, ni kweli vinafaa kwa ngozi yenye mafuta, kuna makala niliandika huko nyuma kuhusu mask ya ndizi, limau na asali kwa ajili ya ngozi zenye mafuta. Ni bora ukiisoma pia.

Anonymous said...

habari! kwanza hongera sana kwa makala yako nzuri kwakweli nimefarijika sana pindi niliposoma makala yako nzuri inayohusiana na jinsi ya kuitunza ngozi yenye mafuta kwani ni mwaka wa ishirini sasa naangaika na vipodozi mbalili bila mafanikio yoyote lakini bado ningeomba unisaidie jambo moja ambalo bado ni tatizo ningeomba unitajie japo aina mbili au tatu ya lotion au kipodozi special kwa ajili ya ngozi zenye mafuta kwani najaribu kuulizia kwenye maduka ya urembo wengi wanaonekana sio wataalamu wa mambo haya bali wako kibiashara zaidi.

Unknown said...

Enter your comment...Thanks for your advice
you knw what you wrote

jerimiah kalisto said...

Uso wang niwamafuta unachunusi na makovu ya sio Isha nitumie nn ili urudie Hali yake ya mwonekano