Thursday, October 8, 2009

Namna ya Kutengeneza Mask ya Avocado


Vinavyohitajika:
1.Avocado moja lililoiva vyema.
2.Mtindi kijiko kimoja cha chakula.
3.Asali asilia (natural honey).
4.Maji ya ndimu/limao.

Namna ya kutayarisha:
Kata Avocado katika vipande viwili, ondoa kokwa na menya.
Changanya avocado ulomenya na mtindi, asali na maji ya ndimu au limao. Koroga mapaka upate mchanganyiko wa hali moja halafu weka pembeni.
Chukua maganda ya avocado na kwa upande wa ndani ya maganda hayo sugulia uso na shingo. Kufanya hivyo husaidia kuondoa seli zilizokufa na ngozi zilizoharibika. Pia huutayarisha uso kwa ajili ya mask.
Kisha paka mchanganyiko uliotayarisha usoni na shingoni (sio machoni).
Subiri kwa dakika 15 na kisha osha kwa maji vuguvugu.

6 comments:

Sophiaclub said...

asante kwa tip nzuri maana namna hii tunatunza ngozi kiasili na ni vizuri kwa afya zetu.

Shally's Med Corner said...

Yeah, karibu sophia.

Anonymous said...

Samahani napenda kujua kama mask hii itanifaa mim mana nina ngozi ya mafuta na hutoka chunusi kiasi.

Nitafurahi kama utanijibu mpenzi...

Mungu akubariki sana na nakutakia kazi njema.

Mdau nipo Musoma

Anonymous said...

Mdau wa Musoma,
kwa bahati mbaya ni bora usitumie maska ya Avocardo kama ngozi yako ni yenye mafuta na kutoka chunusi. Kwani Avocado kwa kuwa na mafuta mafuta, maska ya tunda hilo hufaa zaidi kwa wenye ngozi kavu na za kawaida. Kwa ajili ya ngozi kama yako ni bora utumie mask zinazotengenezwa kwa udongo, ndizi,tango, chai na kadhalika.
Nakuahidi kuwa nitaandika hivi karibuni kuhusiana na namna ya kutengeneza moja ya mask kwa ajili ya ngozi kama yako yenye mafuta.

Anonymous said...

Nashukuru sana kwa maelezo yako..ni mimi mdau wa Musoma.

Mungu akubariki sana

Anonymous said...

Mtindi unaohitajika ni ule ulin chujwa au ambao haujachujwa?