Tuesday, October 6, 2009

Sababu 18 zinazokulazimu upunguze uzito wako na uuogope unene!


1. Unene unaongeza kiwango cha mafuta mwilini, ambayo huongeza uwezekano wa kupata kensa.

2. Unene unaongeza mafuta mwilini, ambayo hufanya matibabu ya kensa yawe magumu zaidi.

3. Unene huongeza mafuta mwilini ambayo huushinikiza nu kuubana moyo.

4. Mtu mnene huwa mvivu kufanya mazoezi, suala ambalo humuongezea zaidi unene.

5. Mafuta mengi mwilini yana madhara kwa ubongo.

6. Unene huathiri hata tabia na miamala ya mtu.

7. Unene huongeza uzito katika mifupa na viunga vya mifupa (bone joints).

8. Unene husababishwa kibofu cha mkojo kibanwe suala linalopelekea matatizo mbalimbali ya mkojo.

9. Unene hupunguza uwezo wa mtu wa kijinsia.

10. Unene hupunguza uwezo wa kuzaa na hata kupelekea utasa na ugumba.

11. Unene hupelekea mwili upatwe kwa wepesi na magonjwa mbalimbali kama vile kisukari na presha.

12. Watu wanene wanapohudhuria mahospitali upimaji wao pia huwa wa matatizo.

13. Unene husababisha ujauzito kuwa wenye matitizo mengi.

14. Unene huathiri pia afya ya mtoto mchanga anayezaliwa.

15. Unene hufanya matibabu ya athma yawe magumu.

16. Unene hupelekea mtu asilale vizuri, na wakati mwingine mtu mnene anapolala hupanwa na pumzi suala linalompelekea kuamka mara kwa mara.

17. Unene humfanya mtu ashindwe kuwajibika vizuri kazini, na hata huweza kuathiri ajira yake.

18. Unene hufanya matumizi ya fedha yawe makubwa.

……Je? Hata baada ya kujua hayo yote bado unaupenda unene?!

3 comments:

Anonymous said...

"duh!! kweli nauchukia unene!!!! kama ndio hivi eeh---sitauhitaji"
hayo ni maneno ambayo nilikuwa nayasema wakati bado sielewi elewi.
Sasa hivi mimi ni mwembamba , yani wananiita toothpick!!
Shida yangu kubwa nataka niongeze uzito kwani sasa hivi nina kilo 50 tu, na urefu wa sentimita 167. Hebu nishauri, uzito na kimo vinafaa?? Na je nawezaje kuongeza uzito ikiwa pia nina condition ya Thyrotoxicosis???

Thanks.
Dallas

Shally's Med Corner said...

Mdau wa Dallas kwanza samahani kwani ndio kwanza naona comment yako. Na naahidi kukupa jibu hivi karibuni.

Shally's Med Corner said...

Mdau wa dallas tafadhali nitumie email yako ili nipate kukupaatia jibu kwa kupitia email.
natanguliza shukrani.