Saturday, October 17, 2009

Utafiti mpya washauri kuwa, watoto wasipewe Paracetamol baada ya chanjo!


Wataalamu wanasema kuwa, kuwapa watoto paracetamol baada ya kupata chanjo ili kuuzia homa, kunaweza kupunguza athari ya chanjo. Utafiti uliofanywa kwa watoto 450 waliopatiwa chanjo umeonyesha kwamba, ni kweli dozi ya paracetamol inapunguza homa kwa masaa 24 baada ya kupewa mtoto, lakini uchunguzi huo umeonyesha pia kuwa, dawa za kupunguza maumivu zina changia kwa kiasi kikubwa kupunguza athari ya chanjo.
Vilevile Madaktari wa Uingereza wameunga mkono uchauri kwamba, haifai kuwapa dawa watoto bila sababu maalum. Kwa hivyo wameshauri kuwa, ni bora wazazi wasiwape watoto paracetamol kabla ya chanjo, kwa kuhofia kuwa huenda wakapatwa na homa baada ya kupatiwa chanjo. Hii ni mara ya kwanza kuonekana athari hiyo na wataalamu wanasema kuwa huenda paracetamol ikawa inaaingilia kati radiamali (response) za seli za kulinda mwili kwa kinga.

2 comments:

mdau wa Ghuba said...

hongera kwa blog yako hii, ambayo inaonekana ni ya kipekee, ya kielimu na siyo ya kichepe kama blog zinbgine za Kiswahili, ambazo mtu akisoma hupatwa na kichefu chefu. Kaza uzi. tuko nawe

Unknown said...

Ahsante mdau wa Ghuba, na karibu sana kona ya Afya.