Wednesday, January 13, 2010

Chai ya kijani yaendelea kupigiwa debe kiafya



Huku chunguzi kemkem zikiendelea kuonyesha faida ya kunywa chai ya kijani au kwa kimombo green tea, wataalamu wa ugonjwa wa kensa wa Chuo Kikuu cha Taiwan wametangaza kwamba, kunywa chai ya kijani kunazuia kensa ya kifua. Utafiti huo unaofanywa kwa kuwashirikisha watu zaidi ya 500 unaongezea nguvu ushahidi unaosema kuwa, chai hiyo ina uwezo wa kuzuia kensa. Katika utafiti huo, watu wanaovuta sigara na wale wasiovuta ambao walikunjwa kikombe kisichopungua kimoja cha chai kijani kwa siku, walipunguza uwezekano wa mapafu yao kupatwa na kensa. Hata hivyo wataalamu hao wamesema kwamba, utafiti huo mpya haumaanishi kwamba sigara sio hatari kwa afya.
Chai ya kijani hutengenezwa kutoakana na majani makavu ya mmea wenye asili ya bara Asia unaoitwa Camellia sinesis, na hunywewa sana katika bara la Asia. Imeripotiwa kuwa kuna idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani barani Asia ikilinganishwa na sehemu nyinginezo duniani, suala ambalo linafungamanishwa na unywaji wa chai ya kijani.

1 comment:

Unknown said...

Nashukuru kwa maelezo kuhusu chai ya kijani. Nimetafuta ripoti hii sbb nina uhitaji wa haraka wa unga huu wa mmea uliouita cmemellia sinesis. Naomba kuufahamu huu mmea kwa lugha ya kiswahili,pia naomba msaada wa jinsi ya kuupata hapa tanzania. Aidha iwe mbegu au km unafaa kukata na kuotesha km baadhi ya maua.