Thursday, January 21, 2010

Siri ya kuishi maisha marefu


Kundi moja la wataalamu wa moyo limeelezea masuala muhimu ambayo yanamsaidia mtu kuishi maisha marefu kama ifuatayo:-
1. Jiweke mbali na sigara.
2. Epuka unene.
3. Fanya mazoezi.
4. Kula lishe bora.
5. Hakikisha unacheki na kupima kiwango cha kolestero mwilini, shinikizo la damu na sukari na kuhakikisha viko katika kiwango kinachotakiwa.
Uchunguzi huo umeonyesha kwamba watu wengi umri wa kuanzia miaka 50 ambao wanaishi kwa kufuata masharti hayo huwa na uwezo wa kuishi miaka 40 zaidi bila kupata shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo, ambayo ni magonjwa makuu mawili yanayoua watu zaidi duniani. Wataalamu wamesema kwamba, kila mtu anayetaka kuishia maisha marefu anatakiwa kufuata ushauri ufuatao:
• Jiepushe kuvuta sigara au acha kuvuta sigara kabisa.
• Hakikisha BMI yako haizidi 25.
• Kila wiki pata dakika zisizopungua 150 za kufanya mazoezi ya kawaida.
• Jitahidi kufuata maelekezo ya kula lishe bora ambayo ni: vikombe 4 na nusu vya matunda na mboga mboga kwa siku, samaki mara mbili au tatu kwa wiki. Usinywe sana vinywaji vyenye sukari, kula vyakula vyenye ufumwele kila siku na chumvi isizidi miligram 1,500 kwa siku.
• Kiwango cha kolestero au mafuta katika damu yako kisizidi 200.
• Shinikizo lako la damu lisiwe zaidi ya 120 chini ya 80.
• Sukari katika damu iwe chini ya 100.

1 comment:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kuna kamsemo fulani huwa nakapenda sana: Eat right, exercise, DIE ANYWAY!

Natania tu mkuu. Mambo uliyoyataja ndiyo ya msingi kwa wanaopenda kuishi maisha marefu.

Kuna mwanafalsafa mmoja aitwaye Epicurus (sijui kama nimepatia jina lake kwani naandika kwa kuparaza tu). Yeye aliuliza swali: kuna tofauti gani kati ya binadamu anayefariki leo na yule atakayefariki baada ya karne moja ijayo? Swali hili huwa linanifikirisha sana!