Wednesday, December 9, 2009

Kunywa kawaha kunaweza kupunguza hatari ya kupatwa na kensa ya korodani


Utafiti uliofanywa nchini Marekani umeonyesha kuwa, kunywa kahawa kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kensa ya korodani au prostate cancer.
Uchunguzi huo umeonyesha kwamba, wanaume wanaokunywa kahawa kwa wingi, hunguza hatari hiyo kwa asilimia 60 ikilinganishwa na wanaume ambao hawanywi kahawa kabisa. Kahawa inaathiri jinsi ambavyo mwili unayeyusha sukari, pamoja na kiasi cha homoni za jinsia, masuala ambayo yanahusiana moja kwa moja na kensa ya korodani. Watalamu hao wamesema kuwa, kampaundi za kibayolojia zilizoko katika kahawa zinazuia tishu kuharibika na hivyo kupunguza uwezekano wa kensa ya korodani kukua.
Inafaa kufahamu kwamba, kensa ya korodani ni kensa ya pili inayowapata kwa wingi wanaume duniani na kusababisha vifo. Kati ya wanaume 6 mmoja kati yao hupatwa na saratani ya korodani.

4 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Lakini kahawa hiyo hiyo inasemekana inaweza kukuletea shinikizo la damu kwani caffeine - kemikali mama katika kahawa ina madhara pia katika mwili. Tufanyeje Dkt?

Shally's Med Corner said...

Kuna ukweli katika unayoyasema Masangu, lakini watafiti hawanabudi kusema yale waliyogundua katika uchunguzi wao.Ingawa kuna baadhi ya wakati chunguzi zinapingana lakini haina maana hazina umuhimu.Na katika tiba inabidi kuchagua lile lililo na umuhimu zaidi. Nitakupa mfano, mtu ambaye katika familia yake kuna ugonjwa wa kensa ya korodani,na kuna uwezekano mkubwa naye akapata ugonjwa huo, ni bora anywe kahawa, kwani pengine itamzuia, na kwa upande mingine, ajitahidi kupunguza uzito wake, asiwe na mafuta mengi mwilini na afanye mazoezi kila mara, kwani shinikizo la damu husababisha kwa kiasi kikubwa na masuala hayo, na kahawa ni kwa kiwango kidogo tu.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Nimekupata Dkt. Hapa Marekani kuna ushauri mpya wa kiafya wa mara kwa mara kiasi kwamba ukifuatilia sana unaweza kuchanganyikiwa. Leo watasema mvinyo nyekundu ni nzuri kwa afya ya moyo, halafu baada ya mwezi mmoja utafiti mwingine unatoka na kusema mvinyo nyekundu hiyo hiyo inasababisha aina fulani ya saratani. Kidogo mtu wa kawaida unachanganyikiwa. Naandika makala kuhusu jambo hili na nikiimaliza basi nitakutumia kabla sijaiweka katika blogu yangu ili uisome na unipe maoni yako.

Siwalaumu wanasayansi kwani lengo lao ni kutuhabarisha kuhusu kile wanachokigundua - ambacho hawatwambii ni kile tunachopaswa kufanya hasa tafiti zao zinapokinzana.

Shally's Med Corner said...

Sawa Bw. Masangu, nasubiri kwa hamu makala yako na ahsante kwa ushirikiano.