Wednesday, December 30, 2009

Sukari kupimwa kupitia lensi za machoWanasayansi wamegundua teknolojia mpya itakayowezesha kupimwa kiwango cha sukari katika damu bila ya kuhitajia mgonjwa kutolewa damu kila siku. Wataalamu hao wa Chuo Kikuu cha Ontario magharibi huko Hamilton, wamegundua teknolojia hiyo mpya ambapo sukari huweza kupimwa kwa kutumia lensi za macho za aina ya hudrogel zilizotengenezwa kwa vipendo vidogo vidogo vya nano. Wagonjwa wa kisukari watakaovaa lensi hizo wataweza kujua kuhusana na kiwango cha sukari mwilini mwao, kutokana na mabadiliko ya rangi ya lensi hizo za macho. Vipande vya nano vilivyotumika kutengeneza lensi hizo, hubadilika kwa kuzingatia molekuli za glukosi zilizoko kwenye machozi, suala ambalo husababisha mabadiliko ya kikemia na mabadiliko ya rangi. Wanasayansi wana matumaini kwamba, kwa kugunduliwa lensi hizo mpya na kuanza kutumika, katika siku zijazo kutakuwa hakuna tena haja ya wagonjwa wa kisukari kudungwa sindano na kuchukuliwa damu kila siku ili kujua kiwango cha sukari mwilini.

No comments: