Friday, January 29, 2010

Vidonge vya kuzuia mimba baada ya siku 5 vyaingia madukani


Vidonge vya kuzuia mimba kwa dharura (the morning after pills) zimeingia madukani, ambapo inaaminiwa dawa hizo zina uwezo wa kumzuia mwanamke asipate mimba hata baada ya kuzitumiwa ikiwa siku 5 tayari zimepita baada ya kujamiina. Uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa Uingereza umegundua kuwa, daw ahizo mpya zina uwezo zaidi wa kuzuia mimba kuliko zile za zamani ambazo zilikuwa zikizuia mimba hadi baada ya siku tatu tu toka wakati wa kufanya mapenzi. Kwa kawaida dawa za kuzuia mimba kwa dharura au emergency contraception zinatumia homoni ambazo aidha huzuua yai lizitoke katika ovari masaa kadhaa baada ya kujamiiana, au kuzuia yai lisijikite katika mfuko wa uzazi.
Si vibaya hapa nielezee vidonge vya kuzuia mimba kwa dharura ni dawa za aina gani?
The Morning after pills ni vidonge ambavyo huzuia mtu asipate mimba iwapo hakutumia njia yoyote ya kuzuia mimba kabla au wakati wa kufanya tendo la ndoa. Ingawa dawa hizo zinajulikana kwa vidonge vinazotumiwa asubuhi kama lilivyo jina lake lakini kihakika dawa hizo huwa na uwezo wa kumzuia mtu asipate ujauzito kwa muda wa masaa 72 au siku 3 kwa kawaida (Huku zile mpya nilizoungumzi hapo juu zikiweza na uwezo wa kuzuia mimba hadi siku 5). Lakini dawa hizo kila zinapotumiwa mapema zaidi baada ya tendo la ndoa, matokeo yake huwa bora zaidi. Vidonge hivyo hufanya kazi vizuri zaidi vinapotumiwa katika masaa 12 baada ya kufanya mapenzi bila kujikinga. Dawa hizo huwa zina homoni inayoitwa Lovenorgestrel ambayo ni moja ya vitu vilivyoko katika vidonge vya kawaida vya kuzuia mimba (contraceptive pills). Unaweza kuapata vidonge hivyo katika vituo vya afya au mahospitalini.
Uingereza na katika nchi nyingi za Ulaya vidonge hivyo huitwa 'emergency contraceptive pill' wakati Wamarekani na nchi nyinginezo huviita 'The Morning After Pill'.
Viodnge vya kuzuia mimba baada ya kujamiina kwa kawaida husaidia kwa asilimia 100 kutopata mimba, na kushindwa kwake ni kwa asilimia chache.
Vidonge hivyo vinatumika katika masuala mbalimbali kama vile:
1. Kuwazuia kupata mimba wanawake waliofanya mapenzi bila kujikinga kabla au bila kutumia kizuizi chochote wakati wa tendo la ndoa.
2. Kwa wale waliobakwa, na kuna hatari kwamba wanaweza wakapata mimba.
3. Kwa mke na mume au wale wapenzi ambao wakati wa kujamiiana condom ilipasuka.
4. Kwa wale waliofanya ngono zembe kwa kushawishiwa, wakiwa wamelewa au kutumia madawa ili kuwazuia wasibebe mimba.
Kumbuka kuwa, hakuna hatari yoyote kutumia dawa hizo. Lakini ni bora upate ushauri wa mtaalamu kabla ya kutumia. Ni asilimia chache sana ya wanawake ambao hupata matatizo madogo madogo baada ya kutumia dawa hizo kama yale wanayoyapata wakati wa kutumia vidonge vya kuzuia mimba vya kawaida. Matatizo hayo ni kama vile.
Maumivu ya kichwa kidogo.
Tumbo kuuma kidogo
Maziwa kuuma kidogo.
Kuona matone ya damu kidogo.
Kujisikia kizunguzingu kidogo.
Ni muhimu pia kujua kuwa, kuna wanawake ambao hawaruhusiwi kabisa kutumia dawa hizo na hao ni wale ambao wana matatizo ya figo au wale wenye matatizo yanayoitwa porphyria.
KUMBUKA KUWA KUZUIA MIMBA NI BORA KULIKO KUTOA!
Na daima tunza Afya yako!

18 comments:

Anonymous said...

Kwa tanzania vipo kweli???

neema mwansasu said...

Ndio vipi kwenye maduka ya Dawa na vinajulikana kama P2


Anonymous said...

vinauzwa shilingi ngapi

Anonymous said...

p2 ni shiling ngap

Anonymous said...

p2 ni shiling ngap

Unknown said...

5000

Unknown said...

5000

Dwayne Gerry said...

Je ukinywa cha kwanza then kidonge cha pili ukapitiliza mda kidogo yaani baada ya hayo masaa 12 kama ilivyo elekezwa vidonge hivyo vitafanya kazi!?

Dwayne Gerry said...

Je ukinywa cha kwanza then kidonge cha pili ukapitiliza mda kidogo yaani baada ya hayo masaa 12 kama ilivyo elekezwa vidonge hivyo vitafanya kazi!?

Lucie said...

Ili kujua masaa 72 inatakiwa kuhesabu pale tendo lilipotokea au inakuaje ? Naomba ufafanuzi

Anonymous said...

Yap 72 hrs soon after having sex....

Mimit said...

Zikipita masaa 72 unafanyaje

Unknown said...

Ukiwa umekunywa mfano mchana alafu usiku ukasex na ukagundua ni siku ya hatari
Je kuna uwezekano ukapata mimba

Unknown said...

Mimi nimekunywa na nimepata mimba

Unknown said...

Mmmh p2 ndo inazuia baada ya siku 5 au??

Unknown said...

na je kuna aina ngap za p2 cz kuna p2 ina vidonge vinwili n nyingine kimoja je matumizi yake n sawa au?????

Anonymous said...

Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159

Anonymous said...

Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* bahati nzuri
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159