Sunday, November 1, 2009

Idadi ya watu wanaokufa kutokana na homa ya mafua ya nguruwe duniani yaongezeka


Twakimu za hivi karibuni kabisa za Shirika la Afya Dunian WHO zinaonyesha kwamba, zaidi ya watu 700 wanakufa kila wiki kutokana na homa ya mafua ya nguruwe!
Zaidi ya vifo 5,700 viliripotiwa Oktoba 25 ikilinganishwa na vifo 5,000 vilivyotokea wiki moja kabla.
Watu wengi wamefariki zaidi katika maeneo ya Amerika ambapo zaidi ya vifo 4,175 vimeripotiwa. Baadhi ya nchi kama vile Ukraine vimefunga mashule na kupiga marufuku mikusanyiko ya hadhara kama njia ya kukabiliana na mfumuko wa ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe hasa katika msimu huu wa baridi. WHO imetangaza kwamba, nchi nyingi hazihesabu tena watu wanaopatwa na ugonjwa huo na kwa sababu hiyo basi inakadiriwa kwamba watu walioambukizwa virusi vya H1N1 ni wengi sana duniani.
Ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe ulianzia nchini Mexico April mwaka huu, na hivi sasa ugonjwa huo umeenea katika nchi nyingi duniani, suala lililopelekea ugonjwa huo kutangazwa kuwa janga la ulimwengu.
Kona ya Afya inawahusia wadau wa globu hii kuzingatia kuosha mikono vizuri kwa sabuni kila mara na kuvaa mask wanapokuwa kwenye mikusanyiko ili kujiepusha kupatwa na homa ya mafua ya nguruwe. Naahidi kuwa hivi karibuni niaelezea kwa kina kuhusiana na ugonjwa huo. Tuzilinde Afya zetu!

2 comments:

Born 2 Suffer said...

Kusema kweli wadhungu ni watu wachafu sana yani, Hio ngozi yao nyeupe ndio inawasaidia lakini hawana usafi kabisa.

Shally's Med Corner said...

mtizamo wako huo, unafurahisha kweli Born to suffer..lol...sijui labda ni kweli!