Friday, November 13, 2009

Mshituko wa Moyo ( Heart Attack) au Myocardial Infarction….sehemu ya kwanzaMshituko wa moyo unatokea wakati mzunguko wa damu katika misuli ya moyo unapozuiwa. Iwapo mzunguko huo wa damu hautoendelea haraka, kitendo hicho huifanya misuli ya moyo kuharibika kwa kukosa oksijeni na huaza kufa. Mshituko wa moyo kwa lugha ya tiba unajulikana kama 'Myocardial Infarction' inayomaanisha "Myo".. muscles au msuli, 'cardio'…. Heart au moyo, "infrct"….death of tissue from lack of oxygen au kufa tishu kwa kukosa oksijeni.
Kama vilivyo viungo vingine mwilini hasa misuli, moyo nao huhitajia damu. Bila damu seli za moyo hudhoofika suala ambalo hupelekea mtu kuhisi maumivu. Shinikizo la damu hutokea pale mshipa mmoja wa damu au zaidi inaposhindwa kusafirisha damu yenye oksijeni katika moyo, kutokana na kuziba mishipa hiyo. Mishipa ya damu inaweza kuziba kutokana na:
1. Kuta za mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo (coronary arteries) kuwa nene.
2. Chembechembe za mafuta kukusanyika katika mishipa ya damu.
3. Kudhoofika na kukonda mishipa ya damu.
4. Mishipa ya damu mara inaposinjaa na kushikana au spasm.
5. Kujitokeza donge la damu katika mishipa ya damu.

Lakini ni wakati gani mtu anakabiliwa na hatari ya kupata mshituko wa moyo?
• Kuongeza umri au umri mkubwa
• Unene wa kupindukia
• Kuvuta sigara
• Shinikizo la damu
• Maisha yasikuwa na harakati na kujishughulisha (sedentary lifestyle)
• Kiwango cha juu cha mafuta katika damu ( High Blood Cholesterol)
• Kisukari
• Kuwa na mawazo, wasiwasi na fikra nyingi.
• Baadhi ya magonjwa ya moyo.
• Kufanyiwa operesheni ya moyo.
• Kuwa na ndugu ambao wana matatizo ya moyo.
• Wanaume.
……msikose kuungana nami katika sehemu ya pili ambapo tutajadili kwa undani sababu hizo na mengineyo.

2 comments:

Anonymous said...

Naisubiri kwa hamu sehemu ya pili ya maelezo yako. Nimefurahi kuipata Blogi yako, namshukuru Mungu.

Unajitahidi kueleza vitu vigumu katika lugha inayoeleweka. Nimekuelewa vizuri sana. Ahsante sana.

This Is Black=Blackmannen

Shally's Med Corner said...

Karibu sana mdau (Blackmannen)katika blog yako hii ya Afya. Naahidi kutochelewesha sehemu ya pili ya mada hii.
Karibu sana!