Friday, November 6, 2009

Namna ya Kujikinga na Homa ya Mafua ya Nguruwe….Sehemu ya Pili1. Vaa mask za uso ili kujikinga kupata ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe, hasa unapokuwa katika maeneo ya mikusanyiko.
2. Ziba pua na mdomo pale unapokohoa au kupiga chafya, ni bora ukitumia soft tissue ( karatasi za kufutia uso). Tupa katarasi hiyo baada ya kutumia mara moja tu. Ni bora ujiepushe kutumia vitambaa kwani kitambaa hutumika mara kadhaa na huweza kusadia kubeba vijidudu.
3. Ni bora ujiepushe kwenda kwenye mikusanyiko isiyo ya dharura, kwani sehemu kama hizo huweza kuwa mazingira mazuri ya kuambukizana homa ya mafua ya nguruwe.
4. Dumisha usafi, osha mikono na uso vizuri kwa sabuni mara kwa mara. Suala hilo hupunguza maambukizo ya virusi vya mafua ya nguruwe. Ni bora iwapo utatumia sabuni za kuua vijududu kama vile dettol n.k.
5. Waangalie vyema watoto kwani wao vi rahisi kupata ugonjwa huo. Wafundishe kuosha mikono kila mara na kudumisha usafi na ni bora kama watapata kinga ya ugonjwa huo.
6. Jiepushe kula hovyo, hasa vyakula vya vinavyotayarishwa nje ya nyumba, kwani huenda vikawa si salama na vikakusababishia kuambukizwa virusi vya mafua ya nguruwe.
7. Kunywa maji yaliyochemshwa.
8. Jiepushe kuwashika au kuwa karibu na nguruwe, ni bora wanyama hao watengwe ili kuepusha maambukizo ya ugonjwa huo.
9. Iwapo utajisikia dalili za mafua au dalili nyinginezo za homa ya mafua ya nguruwe ni vyema umuone haraka daktari.

No comments: